Followers

Idara ya Uhamiaji yafunguka kuhusiana na uraia wa Kidao



Idara ya Uhamiaji nchini imesema inaendelea na uchunguzi juu ya uraia wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara hiyo, Ally Mtanda, amesema bado wapo kwenye uchunguzi na pale utakapokamilika watakuwa na majibu sahihi ya kusema.

"Bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na suala hilo, pale utakapokamilika tutakuja na majibu sahihi ya kusema, kwa sasa bado haujakamilika" alisema Mtanda.

Hatua hiyo ilikuja mara baada ya kuelezwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu huyo hana uraia wa Tanzania.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.