IS wasambaza video za mauaji ya wanajeshi wa Marekani
Wapiganaji wa kundi la Islamic State
IS wamesambaza picha za video zinazodaiwa kuonyesha mauaji ya wanajeshi
wane wa Marekani waliouawa nchini Niger mwezi Octoba mwaka mwaka jana.
Picha hizo zilipigwa na mmoja wa wanajeshi wa Marekani kupitia kamera yake ya siri aliyokuwa nayo kwenye kofia yake ngumu aliyokuwa ameivaa yaani Helmet.
Lengo la video hizo ni kutaka kubainisha kwamba IS ndiyo waliofanya shambulio hilo.
Picha zinazo onekana zinaanza na zile za mnato ambazo baadhi ya wapiganaji hao wakitoa kiapo cha utii kwa kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi mtandao huo wenye makundi yenye utiifu kwa IS kama vile Sahel, Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM).
Kwa mjibu wa BBC video hizo zinawaonyesha wapiganaji hao wakitembea na kukimbia jangwani kuelekea kufanya shambulizi.
No comments
Post a Comment