Madaktari Wamchoma Mtoto Sindano Kichwani Kimakosa Chaanza Kuoza
Stori ninayokusogezea ni kuhusu matukio ya kutokuwa makini katika idara ya afya hasa kwamadaktari yanazidi kuzua wasiwasi kwa wananchi nchini Kenya, tukio lililotokea siku za hivikaribuni ni la mtoto kuchomwa dawa isiyofaa na kumfanya aanze kuoza kichwa.
Tukio hili lilianyika katika hospitali ya Malava General Hospital katika jimbo la Kakamega nalilitokea huku kukiwa na kesi dhidi ya Madaktari wa hospital ya Kenyatta baada ya Daktarikumfanyia upasuaji mgonjwa asiyestahili.
Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Clinton Luchivya alikuwa amepelekwa katika hospitalihiyo baada ya kuwa mgonjwa na madaktari kumchoma kichwani baada ya kukosa mshipa wakumwekea dawa.
Kulingana na mama wa mtoto huyo, mwanae alikuwa na ugonjwa wa Malaria kabla ya kupokea matibabu katika hospitali hiyo. Alisema kuwa mwanae alikuwa ameanza kubadilikabadilika kabla ya kufahamu kuwa kichwa chake kinaoza.

No comments
Post a Comment