Mbunge Uganda: "Kama mwanaume lazima, umuadhibu mke wako"
Mbunge wa Uganda amewaacha watu na butwaa baada ya matamshi yake yaliyoonekana kuunga mkono wanawake kupigwa na waume zao.
Twinamasiko Onesimus, anayewakilisha jimbo la Bugangaizi Mashariki alisema manaeno hayo yakushangaza akiwa katika mahojiano na kituo cha televisheni cha NTV Uganda.
- Tanzania kupiga vita ukatili wa kijinsia
- Je, kuna ufahamu juu ya unyanyasaji wa wanawake usafiri wa umma Tanzania?
- Unyanyasaji kingono wa wabunge wanawake umezidi, ripoti inasema
"Kama mwanaume lazima umuadhibu mke wako mguse kidogo, mkamate na umnyooshe vizuri"
Kipande hicho cha video kilisambazwa na mwandishi wa NTV kwenye mtandao wa Twitter na watu hawakusita kutoa maoni kwa haraka.
Bala Davis anauliza ' je na mwanamke pia anafaa kumchapa mwanaume?'
Wakati Issa Kato kauliza 'je, huyu hajakiuka taratibu za kibunge?
Inaonekana kama Bw Onesimus aliyeoa alikuwa anajibu tamko alilolitoa Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwenye siku ya wanawake , aliposema wanaume wanaowapiga wake au wapenzi wao ni "waoga"
"Wanaume wanaowapiga wanawake ni wapumbavu na waoga" aliwaambia watu katika sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Kikristo cha Uganda.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor , zaidi ya moja kati ya wanawake watano kati ya umri wa miaka 15 hadi 49 wamepitia unyanyasaji wa majumbani na kingono nchini Uganda.
No comments
Post a Comment