MGODI wa dhahabu katika Kijiji cha Nyamitondo wilaya na mkoani Geita umefungwabaada ya raia wawili wa China kufariki ndani ya shimo lenye urefu wa zaidi ya mita 100 kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivunja miamba.
Wachina hao, imeelezwa, walikuwa wakivunja miamba ya dhahabu katika mgodi huobila ya kuwa na vyeti vya kulipiua baruti.
Mgodi huo unamilikiwa kwa ubia baina ya Mayala Ngweso na kampuni ya Kichina ya Taichangain Tanzania Group.Akitoa tamko la kufunga mgodi jana, Afisa Madini MkaziMkoa wa Geita, Alli Maganga alisema hatuahiyo inalenga kupisha uchunguzi wa kina.
Pia, alisema Maganga, hatua hiyo itashinikiza mgodi huo kutekeleza masharti namaelekezo uliopewa na serikali ili kuhakikisha sheria na kanuni za madinizinazingatiwa na kufuatwa.
Maganga alisema raia wawili wa China waliotambuliwa kwa majina ya Li Shaobin (44) naQian Zhaorang (49)waliojitambulisha kuwa mafundi michundo walifariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya na baruti ndani ya shimo katika mgodi huo wakilipua miamba ya dhahabu.
Alisema uchunguzi wa awali ulibaini marehemu hao hawakuwa na vyetivinavyowaruhusu kulipua baruti, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria ya nchi.
Idara ya Madini ilifahamu kuwapo kwa tukio hilo baada ya uongozi wa mgodi kutoataarifa ya ajali hiyo kwa mamlaka husika, alisema Maganga, Maganga alisema Sheria ya Baruti nchini inazuia mtu yeyote kulipua baruti bila ya kuwa na kibali.
Awali, akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Lotson alisema chanzo cha ajali ni uzembe na kutahadharisha wamiliki wamigodi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na tahadhari ili kupeukana na jali zisizo za lazima.
Oktoba 10, mwaka jana mchimbaji mmoja alifariki dunia na mwingine kunusurikabaada ya kufukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi wa dhahabu usio rasmi waBingwa, katika kijiji cha Rwamgasa wilaya na mkoa wa Geita usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Lodson, alimtaja aliyefariki kuwa ni FikiriPaulo (27), mkazi wa kijiji cha Mlanda wilayani Chato ambaye mwili wake ulitolewashimoni akiwa ameshaaga dunia.
Mwili huo ulitolewa shimoni na wachimbaji wadogo, kwa mujibu wa mkurugenzi wamgodi wa Bingwa, Hussein Nyanzala.
Nyazala alisema walikesha wakiendesha zoezi la kuufukua mwili wa marehemu kuanziasaa 5:00 usiku ajali ilipotokea hadi saa moja asubuhi.
Kamanda Mponjoli alimtaja manusura wa ajali hiyo kuwa ni Musa Evarist (19), mkazi wakijiji cha Mpomvu.Alisema Evarist aliokolewa muda mfupi baada ya kufukiwa na kifusiwakati wakichimba mwamba.
Chanzo cha ajali hiyo kilidaiwa kuwa ni kukatika kwa gema la udogo wa mwamba wamawe katika shimo walimokuwa wakichimba vijana hao, Baada ya gema kukatika, imeelezwa, kifusi kilifukia wachimbaji hao.
No comments
Post a Comment