TABORA: JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO SIKUKUU YA PASAKA
Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limezipiga marufuku kumbi zote za starehe na waandaji wa Show/Disko Toto kwenye Sherehe za sikuku ya Pasaka siku ya Tarehe 01/04/2018 siku ambayo watanzania wataungana na wakristo wote duniani kusherehekea sikukuu hiyo ya Pasaka
Lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha usalama wa wananchi na Mali zao unakua salama katika kipindi chote cha sikukuu.
Vilevile Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wazazi wote kua makini siku hiyo ya Sikukuu kwa kutoa uangalizi maalumu kwa watoto pindi wanapo waruhusu kwenda matembezini. Na ikiwezekana wasiwaruhusu watoto kutoka Pekeyao kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wao kwa vyombo vya moto kama Bodaboda,Bajaji n.k ambavyo siku za sikukuu hua bize na hawachukui tahadhari
Akizungumza na waandishi wa Habari kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Wilbrod Mutafungwa amesema kua
"Licha ya kujidhatiti kiulinzi Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora lakini pia nawaomba wakazi wote wachukue tahadhari pindi wanapotoka kwenda matembezini au kwenye nyumba za Ibada kuhakikisha wanaacha waangalizi wa Mali nyumbani kuliko kuondoka familia nzima kuhatarisha usalama wa Mali zao" Alisema

No comments
Post a Comment