UVCCM YAMVAA WAZIRI SHOZA KUFUNGIWA KWA WASANII
Supernidablog
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James ameshutumu vikali kitendo cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufungia kuchezwa kwa nyimbo 15 za wasanii wa Tanzania kutokana na nyimbo hizo kudaiwa kuwa hazina maadili.
Akizungumza leo wanachama wa umoja huo wa vijana, Kheri amewataka viongozi wenye jukumu la kusimamia tasnia ya muziki kuacha kufanya kazi ya uhakimu na badala yake wasimame kama walezi na walimu.
Katika maelezo yake ya leo, James amesema siku za hivi karibuni wameshuhudia baadhi ya kazi za wasanii zikifungiwa kwa kigezo cha sheria na taratibu.
“Ujumbe wangu kama mwenyekiti wa chama hichi kinachoongoza dola viongozi wanaoshughulika na masuala ya sanaa na utamaduni wasiifanye kazi hiyo ni kazi ya uhakimu bali waifanye kazi ya ualimu ya kufundisha watu namna ya kuendana. Serikali ya CCM imeahidi ajira kwa vijana ambazo zinatokana na kuajiriwa na kujiajiri wenyewe na kwamba kuna vijana wameamua kushiriki katika kazi za sanaa kwa kujiajiri tika sanaa, wajibu wetu ni kuwawezesha na kuwasaidia na si kuwakata miguu", amesema“
Ameongeza kwamba kwamba wasimamizi wasitumie kigezo cha sheria na taratibu kuwaaangamiza watu ambao walikuwa na uwezo wa kuwaelimisha na kuwasaidia.
“Leo kuna wasanii ambao wameitangaza vizuri nchi yetu kimataifa lakini pia wameongeza mapato kwa kuchangia kodi kwa kazi zao za sanaa. Sasa leo tumewapoteza ama tunaweza kuwapoteza mabalozi wazuri wa nchi yetu kwa kazi ya sanaa kwa makosa ambayo yanazungumzika pasipo hukumu,” Kheri.
Mwenyekiti huyo amekazia kwamba endapo jumuiya hiyo itaendelea kuwaacha vijana wakiangamizwa kwa kile kinachoitwa sheria na taratibu hakuna atakayebakia. “Leo mtamfungia huyu, keshokutwa mtamfungia yule halafu mnasema mnataka kodi, wale ndio walikuwa wakichangia kodi kwa jasho lao mnawapoteza".
No comments
Post a Comment