Followers

Alikiba, Abdukiba na Zabibu Kiba Ndoa zao Kuongozana Soma


Wengi wamekuwa wakijiuliza sababu ya watoto wa Mzee Salehe Kiba, Ali Salehe Kiba, Abdul Kiba na Zabibu Kiba kuongozana kwenye kuoa na kuolewa lakini hatimaye siri imevuja kuwa, mama yao ndiye aliyechagiza hilo ili kuwapa radhi zake.

Akizungumza na Ijumaa juzikati, mmoja wa wanafamilia ya Kiba aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, Ali Kiba na Abdu Kiba hawakuwa na mpango wa kuoa katika siku za hivi karibuni lakini mkwara wa mama yao ndiyo uliwasukuma kufanya hivyo.

“Kuna wakati mama yao alikuwa hana furaha kabisa na akiulizwa anasema, anaumia kuona wanaye umri unakwenda lakini hawaoi, wanaishia kuonekana na wasichana na kuzaa nao tu, alikuwa akiumia sana.

“Alitamani sana kuona wanaye wanaingia kwenye ndoa haraka na alikuwa akiwaeleza kila wakati kuhusu hilo. Sasa ili kumfurahisha mama yao ndipo wakaamua kuwa waoe tena kwa kufuatana, ndiyo maana unaona ndoa zao zimeongozana. “Na Zabibu naye siku si nyingi anaolewa, ilikuwa naye aolewe baada ya Abdu kisha wafanye sherehe ya harusi ya pamoja lakini kuna vitu vimekwamisha hilo,” alidai mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.