Njegere ni mboga yenye virutubisho vingi vinavyofanya kazi ya kujenga , kuboresha ufanyaji kazi wa ini na ni chanzo kizuri cha Protini.
Ulaji wa njegere mara kwa mara husaidia kuboresha kinga ya mwili, kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu lakini pia huzuia mtu kuzeeka kwa haraka na zina kiwango kidogo cha kalori.
Njegere zina kiwango cha nyuzinyuzi, vitamin A, B na C na hazina mafuta yanayoweza kuganda katika mishipa ya damu.
Lakini pia zina uwezo wa kuzuia saratani ya tumbo. Protini iliyopo katika mboga hii husaidia kuyeyusha damu iliyoganda na kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu, wanatakiwa kutumia njegere zilizochemshwa kila siku.
Ulaji wa njegere za kijani huongeza damu, hukabiliana na udhaifu wa afya lakini zinasaidia kupunguza maumivu katika kidonda kinachouma kwa sababu inasaidia kuondoa asidi zilizopo tumboni.
Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa tiba-lishe wa taasisi moja nchini Marekani, Dkr George Mateljan anasema, njegere ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha kamba lishe zenye uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu inayosababisha shambulio la moyo.
Matokeo ya utafiti wake huo aliouandikia kitabu kiitwacho ‘The World’d Healthiest Foods’, Dkt Mateljan anasema asilimia 65 ya ,begu ya njegere ni kamba lishe ambapo pamoja na kushusha ;ehemu, pia huondoa shinikizo la damu na kuzuia shambulio la moyo.
“Watu wengi wanakula kidogo sana, hawajui faida hizi. Lakini ukweli ni kwamba njegere ni chakula muhimu mwilini hasa kwa wagonjwa wa moyo na sukari,” alisema Dkt Mateljan na kuungwa mkono na mwalimu mwingine Dkt Rafael Nyampinga wa jijini Dar es Salaam.
No comments
Post a Comment