Followers

Dansa Wa Diamond Naye Kakumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto



Dansa kutoka WCB ambaye ni mchezo shoo wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zungu amekumbwa na skendo ya kuwa mmoja kati ya wanaume waliotelekeza watoto wao Dar.

Siku ya jumatatu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwakusanya wanawake wote ambao wametelekezwa na wanaume ambao wamezaa nao ambapo hawawahudumii watoto wao.

Mmoja kati ya Wanawake waliojitokeza ni mwanamke ambaye alijitambilisha kama mzazi mwenza wa Dansa wa  Diamond anayejulikana kama Zungu ambapo alidai alimtelekeza yeye pamoja na mtoto wake baada ta kuachana ambapo amekuwa hataki kumtunza mtoto wake.

Baada ya tuhuma hizo Zungu alitafutwa na Timamu Tv ambapo amefunguka na kusema yule mwanamke ana matatizo ya akili pia ni mkorofi na amedai kuwa hajawahi kumkataa mtoto wake na amesema yupo tayari hata leo kwenda kwa Makonda na kujielezea na kama ikitokea anatakiwa amchukue mtoto wake amesema yupo tayari kumlea mwanaye mwenyewe.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.