Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto na Nandy wahojiwa na Polisi kwa kusambaza video za faragha, wapewa dhamana...
Mwakyembe amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota wa muziki, Diamond ambae tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha.
Pia Mwakyembe amesema pia imebidi binti Nandy naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.
Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria zingine na nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulindwa kizazi cha sasa na cha kesho cha Taifa hili.
Akiuliza swali, mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alitaka kujua kauli ya Serikali juu kukithiri kwa ushoga na kutukana matusi mithili ya bomu la nyuklia ambayo sio maadili ya mtanzania na team za matusi ikiwemo za Wema, Zari, Diamond na Shilole.
Mwakyembe amesema sheria ya EPOCA ilitungwa mwaka 2010 lakini zilikosekana kanuni za kubana maudhui hasa upande wa mitandao. Amesema kanuni zimeshatungwa na zimeanza kufanya kazi.
No comments
Post a Comment