Followers

FATMA KARUME KUHOJI MAMLAKA YA DPP, AAHIDI KUIPIGANIA DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA


Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika-TLS, Fatma Karume amebainisha baadhi ya masuala atakayofanyia kazi katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo kuhoji namna ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na Upelelezi-DPP anavyotumia madaraka yake.

Fatma Karume amesema DPP amekuwa akiwanyima watu dhamana baada ya kuwakamata na kuendelea kuwashikilia kwa madai ya kutokamilika kwa upelelezi, kinyume cha sheria.

Hali kadhalika ameahidi kusimamia demokrasia, haki na utawala bora hapa nchini.

Suala lingine alilosema Fatma Karume, ni kuhakikisha wanasheria wanashirikishwa katika shughuli za kutunga sheria.

Pia, alisema atabadilisha hali ya wanasheria, ikiwemo kuhakikisha kunakuwepo mazingira rafiki yautendaji kazi ili watekeleze majukumu yao vizuri ikiwemo kufanya kazi za uwakili.

CHANZO MWANACHI

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.