Followers

Huhitaji Kusahau Kwamba Wewe Ni Kitu Hiki


Kwenye maisha yako, kuna wakati unakumbana na kukatishwa tamaa, msongo wa mawazo na maumivu makubwa sana, ni rahisi sana kufikiri kwamba huna thamani na dunia ndiyo kama imekugeuka na huna bahati nayo kabisa.

Lakini kwa upande mwingine unaweza ukawa unasahau, hayo yote yanayokutokea ni kweli yanakutokea wewe, na kwa sababu wewe ni binadamu. Hayo hayawezi kulipata jiwe au mti ni wewe na mwingine yanampata kwa wakati wake.

Hakuna njia au namna ya kukimbia. Kama ni maumivu yakabili vivyo hivyo utafika wakati yataisha, kama ni kukatishwa tamaa vumilia, nako pia kutakwisha, hali zote hizo unatakiwa kupambana nazo mpaka uzivuke.

Unatakiwa ujue wewe ni binadamu na yapo mambo mengi ambayo utakutana nayo na ambayo yanakupasa kiuhalisia uwe mvumilivu kukabilina nayo. Kuna wakati kutokana na makosa ya kibinadamu utaumizwa na pia kuumiza wengine pasipo kujua au kwa kujua.

Kuwa binadamu maanake hujakamilika, kwa nini ububujikwe na machozi muda wote na kila wakati kwa sababu ya kuumizwa na watu wengine au kwa sababu ya makosa fulani fulani. Kumbuka wewe ni binadamu hayo yote kukutana nayo inawezekana.

Kwa hiyo unapokuwa unaona kwamba umepoteza thamani yako na ubinadamu wako pia, kwa sababu tu ya yale unayokutana nayo, hapo kumbuka unakosea kwa kiasi kikubwa. Thamani yako haiwezi kushuka ipo pale pale.

Unahitaji kuyafuta mawazo hayo mara moja, kama ulikuwa nayo ya kujiona wewe si kitu, kumbe una thamani kubwa sana ndani yako ambayo haina mfano. Ndani yako wewe, utaendelea kubaki yule yule wewe wa thamani kubwa, pasipo kujali nini kinakutokea.

Inapofika mahali unajiona wewe si mzuri sana kwa yale unayoyafanya, unatakiwa kujikumbusha wewe ni binadamu unaweza kubadilika.

Inapofika mahali ukashindwa, tena ukajaribu ukashindwa, jikumbushe wewe ni binadamu, uwezo wa kushinda unaoa tena na hapo sio mwisho wako.

Inapofika mahali unaona huoni tumaini tena kwenye maisha yako, kumbuka wewe ni binadamu, tumaini jipya unaweza kuliona tena.

Wewe ni wa thamani sana na unaweza kufanya makubwa yoyote, kwa sababu wewe ni binadamu na fursa hiyo unayo. Unaweza ukatumia akili yako na ikakuletea chochote kile unachokitaka kwenye maisha yako.

Wapi unapokwama, kipi kinachokuliza, hicho kitu kisiwe sababu yoyote kwako ya kushindwa, unaweza kubadilisha giza likawa nuru mara moja. Ni wangapi walikuwa kwenye hali duni na sasa hivi maisha yao ni mazuri sana, nawe unaweza.

Ule uwezo ulionao ndani mwako ni mkubwa vya kutosha kama utaamua kuutumia na kuweza kufikia ndoto zako. Huna haja ya kujitilia shaka kwamba hivi kweli mimi nitaweza, ndio unaweza, chukua hatua utaona matokeo yake.

Kama kuna watu wanakusema kwa sabau ya wewe kushindwa, acha waendelea kusema wao ni binadamu na wewe ni binadamu pia, chochote kinaweza kutokea kwenye maisha wasamehe bure, badili maisha yako na kuwa mwingine kabisa.

Kama hujui ni kivipi utabadilisha uwezo wako ulionao ndani mwako na kuweza kukubadilishia maisha yako, endelea kujifunza wakati unafika utajua. Wewe ni binadamu jifunze na utabadilika tu bila pingamizi lolote.

Tunajua mawe, udongo, milima ni vitu ambavyo havibadiliki, lakini wewe ni binadamu, usikalili maisha yako yawe hivyo hivyo milele , utakuwa unajizulumu sana. Maisha yako yana haki ya kupiga hatua, usijizuie kwa kusema aah mimi siwezi tena.

Acha kuishi kwa ndoto na kujisemea mimi mbona maisha yako ya hivivi tu siku zote, wewee, utakuwa unajidanganya na kujipoteza. Unao utajiri mkubwa ndani yako, jenga subira wakati utajiri huo unaousubiri kufumuka mbeleni unakuja.

Wewe ni binadamu na unaweza kubadailika na kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na kwa wale ambao unao wazunguka kwenye maisha yako wakati wote, yote hayo yanatokea kwa sababu wewe ni binadamu.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
                            

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.