Followers

Joyce Kiria na kuolewa ili aweze kuendelea kuishi mjini


Joyce kaongelea kitu ambacho wanawake wengi tunafanya. Unajikuta unampenda mwanamke kwa moyo wako wote na yeye anakudanganya anakupenda unaingia mkenge unatangaza na ndoa.

Watu wanajiuliza sana kwanini ndoa mengi za siku hizi hazidumu. Hiyo ni sababu moja wapo na kubwa zaidi.

Ukiangalia ndoa nyingi zinazovunjika muda mfupi baada ya kufunga ndoa ni mwanamke kushindwa kuvumilia kukaa kwenye hiyo ndoa.

Hakuna jambo la utajifunza kumpenda mtu kwenye ndoa ni kudanganyana tu. Kama ulikaa na mtu zaidi ya miezi sita na akakufanyia kila kitu ila bado moyo ukakataa kumpenda ni ngumu kumpenda hata baada ya ndoa.

Wanawake wenzangu kama unajua humpendi mwanaume upo kwa ajili ya pesa zake usikubali kumpotezea muda na pesa zake kufunga ndoa na wewe. Kula ukishiba futa mdomo kaa pembeni uheme.

Najua wanawake watamind ila Joyce kaongelea ukweli. Wanawake huwa tunatumia uanawake wetu kupata tunachokitaka hata ikibidi kuzaa na watu tusiowapenda kisa tu wametuahidi maisha mazuri endapo tutawapa watoto.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.