Followers

Kama kuna Mwanamke anayetakiwa kupewa ' Tuzo ' ya Kutukuka kwa Kauli yake ni huyu...

Mlio na ' Video Clip ' yake mtanisaidia kuiweka hapa ila itoshe tu kusema kwamba ni Mwanamke miongoni mwa wale ambao jana walienda Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa matatizo mbalimbali ya Kifamilia ili aweze kupata ' utatuzi ' ila alichokisema pale aliwaacha ' hoi ' kila Mtu ila kilipokelewa vizuri sana na Sisi Wanaume kwani ametusaidia kupeleka ujumbe ' Kuntu ' kwa Wanawake wote nchini Tanzania.

Ifuatayo ni nukuu yake ambayo naiweka hapa na ningependa ndiyo iwe sehemu yetu Kuu ya ' Mjadala '....." Natoa lawama zangu kwa Wanaume wote hasa kwa Kitendo chao cha kutupa Pesa / Hela kila mara wanapokuwa wanamaliza kufanya Mapenzi na Sisi Wanawake ( Wapenzi wao ) Vitandani kwani si kitendo kizuri na kinachangia mno kutulemeza Sisi Wanawake na kupelekea kuwa Wavivu na kutojua kujituma zaidi Kimaisha hadi tunakuja kupata matatizo ya Kimahusiano kama haya "

Nadhani kama kuna Mwanamke ambaye anatakiwa kupewa ' Tuzo ' ya Heshima kwa kusema ukweli bila chembe yoyote ile ya ' Unafiki ' basi ni yule Mwanamke aliyekuwepo jana pale Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul C. Makonda.

Najua na nina uhakika Kauli yake hii itakuwa imepokelewa vibaya na kwa hasira na Wanawake wenzake ila kwa Sisi Wanaume huyu Mwanamke Kwetu amekuwa ni ' Shujaa ' namba moja kwani ametusaidia mno kutuwasilishia yale yaliyokuwa yakitusibu kama siyo kutukera kwa muda mrefu hasa ukizingatia kwamba kama ni ' Utamu ' wa ' Kufanyana ' Vitandani tunaupata Wote sasa iweje tuwe tunawapeni Pesa? au kama vipi basi tukubaliane kuanzia leo kwamba wote tuwe na wajibu wa ' Kuhongana / Kupeana ' Pesa / Hela pale tunapomaliza tu ' Kungonoana '.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.