Followers

Madaktari wabaini tatizo Tena kwenye mguu wa Tundu Lissu



Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu leo atafanyiwa upasuaji mwingine katika mguu wake wa kulia, hii ikiwa ni mara ya 20 tangu alipoanza kutibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi mjini Dodoma, Septemba mwaka jana.

Lissu ameeleza kuwa, madaktari wamebaini bakteria katika mguu wake wa kulia hivyo wameamua kumfanyia upasuaji ili kuwaondoa.

Nitafanyiwa upasuaji katika mguu wangu wa kulia ambao uliumizwa sana. Operesheni hii inafanyika baada ya madaktari kubaini bakteria katika mifupa hiyo wamesema wakiunga bila kuwatibu bakteria itakuwa ni tatizo,” alisema Lissu.

Mbunge huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) anayekaribia kumaliza muda wake, yuko katika Hospitali ya chuo Kikuu cha Leuven, nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu ya awamu ya tatu, ambapo baada ya kushambuliwa kwa risasi mjini Dodona, alikimbizwa katika Hospitali ya Dodoma alipopatiwa matibabu ya awanu ya kwanza  na Baadaye akapelekwa Nairobi alipopatiwa matibabu ya awamu ya pili.

Akizungumzia Afya yake, Tundu Lissu alieleza kuwa imeimarika sana naamewashukuru watanzania pamoja na watu wengine wasio watanzania ambao wamekuwa wakijitolea kwa namna mbalimbali katika matibabu yake.

“Niseme tu naendelea vizuri sana. Ninawashukuru Watanzania kwa kunitibu, kwani wenye jukumu la kufanya hivyo wamekataa, lakini watanzania hawajanitupa,” alisema.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.