Followers

Majina 15 ya Kikuyu ya kike na maana yao ya kuchekesha

Mwanamume Mkenya amewachekesha Wakwanya mitandaoni baada ya kupeana majina ya Kikuyu ya kike na maana yao.
Laban Thuo aliorodhesha majina hayo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook siku ya Jumanne, Aprili 17 na kuwavunja mbavu Wakenya kutokana na maana ya majina yao.

Jamaa mmoja kwenye mtandao wa Facebook amewafurahisha watu wengi baada ya kuorodhesha majina ya Kikuyu ya kike na maana yao ya kuchekesha. Picha: Kwa Hisani
1. Njoki: Msichana mwembamba, anayezungumza na watu sana na mwenye bidii. Huwa wakati mwingi hawaolewi na sio wazuri kwa mahaba kitandani.
2. Njeri: Wengi wana miili mikubwa. Wanadanganya sana na wanapandwa na hasira haraka sana.
3. Muthoni: Ni werevu na wenye vipaji tofauti, wanafiki, wasiri, wanaopenda kinaya na wanazungumza na watu sana. Huwa hawawezi kujizuia. Muthoni akipenda, anapenda kabisa.
4. Wanjiku: Wana tabasamu nzuri, wanavutia sana kimahaba na wanapenda kuzungumza sana na watu, wanaweza kuwa wasichana wa kuwatumia wanaume kupata pesa. Wanakasirika haraka sana, wana mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengi.
5. Wangui: Wana kiherehere sana, wanajivuna sana hasa kwa kuwa na ngozi ya rangi ya maji ya kunde. Sio werevu sana na wanaweza kushawishiwa kwa urahisi. Wao huwa na wapenzi wengi.
6. Wambui: Ni watulivu lakini wanafiki. Wanapenda kuzungumza sana na watu na wanajua mambo mengi. Wanaweza kuwa wake wazuri. Huwa hawapendi kutabasamu, wana tabasamu za kuficha hisia na kuficha kuridhishwa kitandani.
7. Wanjiru: Ikiwa una Ciru, basi una shetani nawe. Mkimbie haraka iwezekanavyo.
8. Wangeci: Wanajulikana kucheka kwa sauti ya juu, hawaaminiki. Wangeci akiamua kitu, huwezi kubadilisha mawazo yake.
9. Wangari: Wana tabasamu na wanacheka kwa njia tulivu, lakini ni watu hatari wakiwa hawajaelimika kuhusu mambo ya kisasa. Wako karibu sana kwenye orodha ya kuwa wake wake wema.
10. Nyambura: Wamepewa jina hilo kutokana na mvua. Ukimpata, muite mhubiri amwombee mara moja, mke mzuri. Ni mzuri zaidi, hapendi kutabasamu sana.
11. Mugeci: Ni fisi. Anapenda kuwasengenya watu. Yeye ni mchanganyo wa Mkikuyu na Mluhya. Ni mpishi au Mluhya tu ndiye anayeweza kumuoa.
12. Njambi: Ni mwerevu, anaweza kuwa mke mzuri, ana nguvu na bidii, hawachoki, wanapenda kukaa pekee yao.
13. Wanja: Inamaanisha ‘kutoka nje’. Ni warembo lakini wengi wao ni makahaba. Wana macho na tabasamu za kuzingua mtu.
14. Wangithi: Wana mawazo ya vitu vya kutisha, wana vurugu na wanapenda kupigana. Ni wakaidi na wanawadhibiti sana waume zao.
15. Waitherero: Ni jina linalotokana na kusini. Ni warembo sana, wanapenda kudanganya sana na wengi wao ni waganga ikiwa sio wasagaji.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.