Followers

Mawandaz;Kifo Ni Nini Jiulize na usome kwa umakini sana

DOWNLOAD APPLICATION YA SUPERNIDA KATIKA SIMU YAKO ILI UWE UNAPATA HABARI KWA ULAHISI ZAIDI 
DOWNLOAD HAPA

*KIFO.NI NINI

KIFO ni muondoko usiokua wa kurejea
KIFO ni kwaheri isiyokuwa ya kuonana.

KIFO ni kufichwa bila kutokea tena.
KIFO ni kupotea kwa sura, sauti na mwili bila kuonekana tena.
KIFO ni siri nzito isiyojulikana!

*Eee ndugu yangu.....!*
Tukae tukiyafikiria sana MAUTI.
Ufahari, mahangaiko, mipango, nguvu, cheo na mengineyo yatasimama ghafla siku moja !
Kitashuka kiza kisicho cha kawaida.

 Mungu

Tunakuomba utuhifadhi na utusitiri na ugumu wa siku hiyo.
HEBU tujiulize masuala haya na lifikirie kwa makini katika akili yako kila suala jibu utapata mwenyewe  ;

Mimi ni nani katika hii dunia ?
Nina miaka mingapi hadi sasa ?

Nimebakiza miaka mingapi ?
Nimefanya mangapi kwa ajili ya akhera yangu ?

Maovu mangapi nimetenda kwa kuteleza au kwa kusudi ?
Lini nilitoa chozi kutubu mabaya yangu ?

Lini nilikaa faragha na kumshukuru MUNGU kwa wema anaonitendea ?
Hivi mola akichukua roho yangu wakati huu, nimebeba amali ngapi za kheri zitakazo nisaidia ?
Nitakumbukwa kwa wema gani niliowatendea wanadamu na viumbe wengine ?

*TUZINDUKE NDUGU YANGU, DUNIA  ISITUHADAE TUKAMSAHAU MUNGU.*
*_TUKUMBUSHANE
TUKUMBUKE PIA MUNGU HADHIHAKIWI ANAPASWA KUABUDIWA YEYE PEEKE YAKE

DOWNLOAD APPLICATION YA SUPERNIDA KATIKA SIMU YAKO ILI UWE UNAPATA HABARI KWA ULAHISI ZAIDI 
DOWNLOAD HAPA


No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.