Mawandaz.Kuna mwanaume m'moja ambayo aliowa wanawake wawili.
Mwanamke wakwanza hakuwahi kuzaa mtoto, yaani alikuwa mwanamke tasa wakati wapili alifanikiwa kuzaa watoto wakike sita tena wazuri sana.
Yule mke wapili akawa anamnyanyasa wakwanza kwakutumia kigezo chakuwa mwenzie hazai. Alikuwa anamtukana huku akisema, "we mwanamke tasa, utapaki vitu vyako mda si mrefu na utatimka. Mungu wako ameshindwa kukusaidia."
Baada ya miaka kadha, Mungu akamjibu yule mke wa kwanza. Akapata ujauzito na akazaa mtoto wakiume. Mume alifurahi sana kwa kuwa Mungu akaibariki familia yake kwa mtoto wa kiume. Akamushukuru sana Mungu.
Mke mdogo akaanza kumuonea wivu mwenzie, kwa kuwa mtoto wa kiume alikuwa anapendwa sana na baba yake.
Baada ya miaka 4 mke mdogo akafikiri vya kumuuwa yule mtoto wa kiume.
"lazima atangulie, maana mwenzangu anapendwa sana sababu hili litoto lake!" akajisemea mwenyewe. Akayenda kwa mganga, ile akapewe dawa yakumuuwa yule mtoto. Mganga akampa dawa ya nyoka wakubwa watatu. Akamwambia ayende usiku chumban kwa mtoto akiwa amelala na akeweke ile dawa ambayo mwisho itabadirika kuwa nyoka wakubwa. Ila akahakikishe mtoto yuko pekeyake.
Usiku akayenda na kufanikiwa kuingia chumban aliko lala mtoto, baada ya kuweka dawa nyoka wakatokeya. Akawaamuru wamuuwe yule mtoto kisha akatoka na kuenda kijiji cha jirani kulala huko.
Wale nyoka walivyotaka kum'maliza yule mtoto, wakaona malaika wawili wamesimama alipo lala mtoto. Badala ya kumuuwa wakageuza nakuenda chumba cha watoto sita wa yule mama nakuenda kuwauwa.
Kesho yule mke mdogo alirudi toka kijiji jiran na akakuta mke mkubwa analia na watu wamejaa pale nyumban. Kimoyomoyo akajisemea, itakuwa yule mshenzi kafa, litakoma kuringa. Akasogea na kisha akauliza nini kimetokea. Mke mkubwa akajibu, "nyoka watatu waliingia chumban kwa watoto wako wakike, na wameuuwa watano m'moja yupo hosipitali. Yeye ameumizwa kidogo, amesaidiwa na mtoto wangu wakiume ambao amefanikiwa kuwauwa awa nyoka.
Yule mke mdogo alilia sana kisha alikiri kwenda kwa mganga na lengo la kumuuwa mtoto wa mwenzie, ila hajuwi imekuwaje nyoka kuuuwa watoto zake.
Siku hi ya leo mwezi watatu nakuombea Mungu akulinde, na kila mtutu alio na mipango mibaya nawewe, mapepo ya kishetani nawewe yamurudiye mwenyewe.
Share Tafadhali
No comments
Post a Comment