Followers

Milioni 56,325,000 Zimepatikana Ndani Ya Nusu Saa Waziri Nchemba Ameongoza Harambee


Na; Daniel Otmary

Waziri wa mambo ya ndani Dk.mwigulu nchemba akiwa ndiye mgeni rasmi katika harambee ya uchagiaji wa ujenzi katika kanisa la Romani Katoriki ililopo mkoani Tabora nje ya mji Ipuli amehudhuria katila kikao cha uchangiaji wa nyumba ya ibaada eneo la ipuli Tabora parokia ya familia takatifu ipuli katika kanisa hilo.

waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akiongea na wana Tabora

Waziri aliweza kuambatana pamoja na baadhi ya wabunge wa majimbo katika mkoa wa Tabora na wawakilishi wake katika kikao hicho cha changizo la ujenzi wa kanisa kwa awamu ya pili.

Aidha waziri Mwigulu katika hotuba yake fupi au uhamasishaji wake amesimama na kusema'' Kuwepo na makanisa kwanza kunasaidia kuleta amani zipo sehemu nilipata kutembelea vijijini huko na huko.Mambo ya kishirikina yametawala na ramri karibu kijiji kizima natukumbuke kuwa hao waganga wapiga ramri hutusikiliza kwanza sisi na akisha sikiliza anaibua la kuibua na kuwapa taarifa na watu wana msikiliza ila Mimi naamini ukijipendekeza kwa Mungu kama Mimi kwa kutoa sadaka ya changizo hakika utabarikiwa'' Amesema Waziri Nchemba.

                                

Pia waziri katika hamasisho la changizo la ujenzi ameongeza kwa kusema kwa tafiti yake binafsi isiyo rasimi ameona kuwa mikoa yenye makanisa mengi hata mvua hunyesha bila kukoma huwezi ona shida ya mvua nikiangalia mikoa kama Musoma,Njombe,Iringa, Kagera, Mbeya na Mwanza ni mikoa yenye makanisa mengi na Mvua kamwe haishi kunyesha, lakini kwa upande wa pili mikoa ambayo makanisa ni machache kwa mfano Tabora, Dodoma, Shinyanga, na Simiyu Mvua ni nadra kuziona zinafululiza kwa hiyo ni jambo jema Tabora kuona mawazo na picha harisi ya kanisa kujengwa na ameunga mkono juhudi hizo.

Dk.Nchemba ameweza  kuchangia kiwango cha Tsh.million 10 tasrimu na kuongeza mifuko mia tatu ya cement na nondo, kwa ajiri ya ujenzi, na ameomba kuingia katika kamati kuu ya ujenzi wa Kanisa kwa lengo la kuendelea kutoa mchango zaidi ya hapo.

Waziri mwiguru nchemba amehitimisha changizo hilo katika kanisa la familia takatifu ipuli mkoani Tabora kwa kutaja machangizo yote kwa waliopata nafasi ya kuhuzuria katika shughuli hii, ahadi pamoja na fedha tasrimu ni Tsh.millioni 56 laki Tatu na ishirini na tano na keshi iliyo patikana ni milioni kuminanne laki Tatu na sitini na moja tu.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.