Followers

Mkewe Willis Raburu aweka picha mitandaoni bila ya vipodozi na anapendeza kweli


Mtangazaji wa runinga ya Citizen Willis Raburu alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa dhati Mary Ngami mwaka wa 2017 kwenye sherehe iliyohudhuriwa na watu waalikwa pekee.

Mkewe Willis Raburu ni mrembo hata bila ya vipodozi.Picha: Maryprude Raburu/Instagram

Habari za harusi yake ziliwashangaza baadhi ya wafuasi wake ikizingatiwa kwamba Raburu alikuwa kwenye uhusiano mwingine wa kimapenzi na Sally Mbilu ambaye alikuwa ashamposa.

Hata hivyo, Raburu na mke wake wamekuwa wakionyesha hadharani mapenzi yao kwenye mitandao ya kijamii na kuwa tamanio kwa wapenzi wengi.

Mary Ngami Raburu aliweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya vipodozi na akavutia wafuasi wake wengi.Picha: Maryprude Raburu/Instagram

TUKO.co.ke iliweza kuzuru ukurasa wa Instagram wa Ngami na kukutana na picha za kupendeza zilizomuonyesha akiwa hapajipodoa.

Ngami alikuwa kwenye mazoezi ya kudhibiti uzani wa mwili wake alipoweka picha hizo huku akiwa ametokwa na jasho kweli kweli.

Mary Ngami Raburu aliweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya vipodozi na akavutia wafuasi wake wengi.Picha: Maryprude/Instagram

"Napenda jinsi uso wangu unavyotoa jasho nikiwa zoezini na ninapojipanguza nahisi nikiwa safi kabisa," Ngami aliandika kwa moja ya picha zake

Ngami alidhibitisha jinsi ni mrembo hata bila ya vipodozi kama ilivyo desturi kwa wanawake wengi hasa ' Slay Queens'

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.