Moses Kuria azua mjadala mtandaoni kwa kuonekana na bintiye Uhuru Gatundu
Kuria alikuwa ameenda kutoa hundi za waliofaidika kutokana na Uwezo Fund Gatundu Kusini
Akiandamana naye alikuwa ni Ngina, aliyeonekana kuwa na furaha, ambaye pia ni bintiye Rais Uhuru Kenyatta
Wawili hao walikaribishwa kwa furaha na vifijo na kundi la kina mama la Inuka Women Self Help Initiative
Wakenya walipuuza hafla kamili na badala yake wakamwangazia Ngina, ambaye alikuwa ni mgeni maalum wa Kuria
Moses Kuria azua mjadala mtandaoni kwa kuonekana na bintiye Uhuru Gatundu. Picha/Moses Kuria/Facebook
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria Alhamisi, Aprili 12 alizuru eneo bunge lake kutoka hundi za watakaofaidika kutokana na mradi wa Uwezo Fund.
Kuria alikutana na makundi 17 chini ya mwavuli Inuka Women Self Help Initiative.
Moses Kuria azua mjadala mtandaoni kwa kuonekana na bintiye Uhuru Gatundu. Picha/Moses Kuria/Facebook
Kundi hilo lilianzishwa na Wakfu wa Kenyatta Trust, shirika lisilo la kiserikali ambayo hulenga wananchi maskini, hasa wanafunzi.
Moses Kuria azua mjadala mtandaoni kwa kuonekana na bintiye Uhuru Gatundu. Picha/Moses Kuria/Facebook
"Hili kusaidia makundi hayo, nimejitolea kushirikiana na Inuka ili kuanzisha mradi wa Maisha Kilimo katika Shule ya Msingi ya Kahuguini," alisema Kuria katika akaunti yake ya Facebook Ijumaa, Aprili 13.
Moses Kuria azua mjadala mtandaoni kwa kuonekana na bintiye Uhuru Gatundu. Picha/Moses Kuria/Facebook
Lakini wananchi walionekana kuvutiwa sio na killichokuwa kikiendelea, bali walikuwa wakimwangazia bintiye Uhuru, Ngina.
Tazama walichosema baadhi ya wananchi baada ya mwanasiasa huyo wa Gatundu kuweka mtandaoni picha zake pamoja na Ngina.
Thiong'o Wa Gichuhi: Continue grooming the Kenyatta's, once those kids are big enough, you will be eliminated the way they did the MP who was there before you so that you can be nominated. You are a pawn in a chess game but no one has to live forever so your demise to most of us will be normal, and in fact when it happens I will add an extra wife to my family to celebrate.
PK Mwangi Kimotho: And you were accompanied by Kenya's first Daughter Ngina Kenyatta. Good job Njamba...
No comments
Post a Comment