Followers

Mrisho Gambo msibani kwa Leyla Mtumwa

Arusha.  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anatarajiwa kuongoza mamia ya waombolezaji katika  mazishi ya Mtanzania, Leyla Mtumwa aliyeuawa Uingereza.

Leyla anadaiwa kuchomwa visu hadi kufa Machi 30 mwaka huu na mume wake, Kema Kasambula, nyumbani kwa wanandoa hao, Kirkstall Avenue, Haringey, Uingereza.

Mwili wa Leyla, uliwasili jana ukitokea Uingereza na anatarajiwa kuzikwa leo jioni mjini hapo.

Kwa sasa, kisomo cha hitma kinaendelea nyumbani kwao, eneo la Kaloleni, Arusha.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.