Followers

Mtoto azaliwa baada ya wazazi wake kufariki miaka minne nyuma

Katika hali ambayo imewashangaza watu wengi, inaripotiwa kuwa huko nchini Chinamtoto amezaliwa baada ya wazazi wake kufariki miaka minne iliyopita.

Hii imewezekana kutokana na mwanamke mmoja kupandikizwa kidaktari mbegu na yai vya wazazi hao ili abebe mimba hiyo.

Mwaka 2013 wazazi hao walitoa mayai hayo yaliyogandishwa kwa matumaini ya kupata mtoto kwa kupitia mfumo wa IVFlakini bahati mbaya walipata ajali kabla ya mayai hayo kutumika.

Kabla ya kufariki wawili hao walitoa ruhusa ya mayai hayo kutumika endapo atajitokeza mtu ambaye anataka kubeba ujauzito wa mtoto wao.

“Hii ni ajabu, tunakaa kujadili watoto kutelekezwa?” -Mbunge Selasini

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.