Followers

Ndege kubwa ya abiria kutua uwanja wa ndege Dsm ni hatua kubwa,lakini itufunze kama Taifa kuwa na vipaumbele vyenye tija



Nimeona hapa na pale habari njema juu ya kutua kwa ndege kubwa kuliko zote za abiria kwa sasa duniani katika uwanja wetu wa Dsm(JNIA)

Ndege hiyo kubwa ya abiria aina ya Airbus 380-800(A380-800) ya Fly Emirates imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kushindwa kutua Mauritius kutokana na hali ya hewa mbovu.

Airbus 380-800 ni moja ya ndege kubwa(double deck,wide body,4 engines,jet airliner) ya abiria kwa sasa duniani yenye uwezo wa kuchukua abiria kati ya 510-617 kutokana na "Seat Configuration".

Ikiwa kwenye "three class Configuration" kwa maana ya "First Class,Bussiness Class na Economy Class" ina uwezo wa kubeba abiria 350-620,lakini ikiwa na "One Class Configuration" yaani "Economy Class" tu kama Fastjet kwa huko nyumbani ina uwezo wakubeba abiria 853.

Mpaka March 2018,kampuni ya Airbus ilikuwa na. "Orders" ya kutengeneza ndege 330,na kati ya wateja wake wakubwa ni Fly Emirates ambayo ime-order ndege 162 na mpaka sasa imeshachukua ndege 102.

Ni furaha kwa ndege kubwa kama hii kutua Tanzania,hii inatupa picha kuwa Uwanja wetu sasa,kwa maana ya Runway na Taxiway kuwa na viwango vya juu vya kimataifa kupokea ndege kubwa duniani,licha ya changamoto zake ndogondogo za uchafu wa jengo na ubovu wa Management ya kiwanja(japo naambiwa kwa level ya Management ya TAA kitaifa kuna mabadiliko makubwa,nafuatilia).Hongera JNIA,a previuos home,far away from my home.

Changamoto iliyopo kwa sasa ni eneo la maegesho na "Lounges".Kwa taarifa ni kuwa ndege hiyo imetua na abiria zaidi ya 450 kwa dharura, wakati huohuo ndege nyingine zilizo kwenye ratiba ya kawaida zikiendelea kutua kama kawaida na wote hawa inabidi wahudumiwe na "facilities" ambazo zilizoea kupokea abiria 650 kwa wakati mmoja,sasa ongezeko la ghafla la abiria 450 juu ya 650 wa kawaida,imefanya lounge ya uwanja wa Terminal two kufuraaa.

Matukio kama haya,ndiyo huonyesha udhaifu wetu na mapango yetu ya muda mfupi.Mpaka muda unakwenda na kwa sababu ya mazoea tu,huduma ya uhamiaji na forodha imezidiwa na ndege ya dharura na abiria wake,hivyo kufanya hata wale abiria wasio wa dharura kukwama.Kwa viwango vya kimataifa,abiria anayewasiri anatakiwa kuhudumiwa ktk huduma za uhamiaji na forodha kwa dakika zisizo zidi 60(ikiwa ni uwanja ulio busy kama JFK Int'nal Airport au Schiphol)

Haya ndiyo mambo tuliyoongea kwa muda mrefu juu ya vipaumbele,kwamba unajenga Uwanja Mpanda,sababu mkuu mmoja yupo madarakani,akitoka madarakani harudi tena Mpanda,anahamia sehemu fulani na kuwa mkulima wa zabibu,na hatimaye uwanja mzuri uliojengwa kwa kiwango cha lami unageuka kuwa malisho ya ng'ombe na chanzo cha majani kwa wale wazee wa "zero grazing".

Hivi ndivyo tulivyojenga hoja wakati mchakato wa Ujenzi wa uwanja wa Ikulu ndogo ya 2015-2020 ulivyoanzwa kujengwa,sasa leo,majibu yanapatikana kupitia dharura kama hizi za Fly Emirates na waliotukosoa,wanabaki kututafuta "inbox" na kukumbusha kuwa yale tuliyoandika na kushauri,leo yameonekana kwa vitendo.

Huwezi kuacha vichuguu vinaota kwenye uwanja wa Lake Manyara ambao unashika nafasi ya Tano kwa miruko ya ndege kwa mwaka,kutokana na uwingi wa abiria wanaofuata utalii halafu unaenda kuanzisha mradi mpya wa ujenzi wa uwanja katika eneo ambalo baada ya madaraka yako kuisha,hakuna mruko wa ndege ya kibiashara kwa maana ya ndege ya abiria au mizigo itaruka kuelekea ktk uwanja ulioujenga.

Jambo la mwisho la kujifunza,ni kujiuliza,kwanini Airbus 380-800 itue Mauriutius kwa "route ya kawaida"(Scheduled flights) halafu kwa nchi kama Tanzania,yenye utajiri wa maliasili na vivutio kedekede vya utalii,tunashangilia ndege hiyo kutuwa kwa "dharura".Hii ni aibu,sisi kwenda na kuanza kushangilia kuwa Taifa la kupokea vitu vya "Dharula".

Karibu sana Airbus 380-800 Tanzania,tulizoea kukuona kwenye viwanja vya wenzetu na kukupanda kwa wengine,walau toka umezaliwa 2005,sasa umetua na Tanzania japo haikuwa dhamira yako.Tujifunze kuepuka vitu vya dharura,tudhamirie na tufanye kweli.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.