Followers

Ndoto kwa kiasi kikubwa huakisi hali halisi ya maisha yetu

Eneo zima la mji pamoja na viunga vyake usiku nguvu za umeme zikiwa zimepotea. Picha/HISANI 

Kwa kiasi kikubwa ndoto huakisi hali halisi ya maisha yetu.

UHALISIA WA NDOTO

NDOTO ni maono tuyapatayo tunapokuwa usingizini. Ila maono hayo husemekana kuwa yanatokana na mambo tunayoyawaza au yanayotufanyikia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo basi, ndoto huwa karibu sana na uhalisi wetu wa maisha.

Hivi ni kusema kuwa wengi wetu huyaishi maisha yetu mengi kupitia ndoto zetu tu.

Yaani kwamba, yale tunayoyawaza sio yale maisha yetu halisi tunayoishi. Ikiwa hilo ni ukweli, basi waja wengi hawaishi maisha yao halisi bali wanaishi maisha ya uongo.

Tuseme kwa mfano, kuna msichana au mvulana ambaye unatamani awe mchumba wako, unamuota kila siku. Ila uliyemwoa au kukuoa siye huyo! Je, iwapo utaendelea na ndoto hizo, bila shaka hayo ndiyo maisha yako wala sio yale unayoyaishi!

Hali kama hii ndiyo iliyomkumba Mashaka katika hadithi ya Ndoto ya Mashaka (Ali Abdulla Ali) ambapo huyu Mashaka alikumbwa na hali za ndoto kuangazia alivyotamani maisha yake yawe. Ila, yalikuwa kinyume.

Wetu wengi hujikuta katika hali kama hii maishani wasijue la kufanya. Kwa hakika, ndoto ni njia muhimu ya kutuelekeza kuwazia mambo tunayoyatamani maishani. Ila ni muhimu kujaribu kuzikabili ndoto hizi na kizitimiza ili zisibakie kuwa ndoto tu bali hali halisi ya maisha yetu. Isije kuwa ndoto kama ya Martin Luther King ambayo iwapo haingehuishwa, Waafrika wangebakia katika hali ya kubaguliwa hadi leo.

Ukweli ni kuwa ndoto ni muhimu.

Zinaweza kuwa ufunguo wa kutufungulia maono mapya na uwezekano wake. Kisha tufuate maono hayo hadi tuyatimize kwani penye nia pana njia.

Tusiwe wenye kuzipuuza ndoto zetu au matamanio yetu ya maisha.

Kwa kweli hapo hatutakuwa tunayaishi maisha kikamilifu. Au pia tusibkie tu katika ndoto bila kujaribu kutimiza hayo tunayoyaota. Huo ni uvivu mkuu.

Hebu fikiria iwapo utaishi miaka yote kukitamani kitu. Bila shaka heri ufe katika harakati ya kukitafuta kuliko kukaa tu bila hata kujaribu. Kwa kutojaribu, utakuwa kama ambaye hujayaonja maisha hata tone moja. Huo bila shaka ndio utamu wa maisha yenyewe!

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.