Ofisa Chuo Kikuu asimamishwa Kazi kwa kumdhalilisha kijinsia Mwanafunzi
KISUZE EDWARD ambaye ni Ofisa Utawala Mwandamizi Ofisi ya Usajili wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, amesimamishwa kazi kwa kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi wa kike.
Barua ya kusimamishwa kazi.
Barua iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. William Bazeyo, kwenda kwa mtuhumiwa, imemsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo ambapo pia hatakiwi kufika katika ofisi hizo.
Mlalamikaji, Njoroge Racheal, aliiambia polisi kwamba Kisuze alimbusu kwa nguvu kwenye mapaja yake na kumshika sehemu za siri.
Mwanafunzi huyo alitumia simu yake kupiga picha kadhaa za tukio hilo ambazo amezifikisha polisi.
Katika maelezo aliyoyatoa polisi, mwanafunzi huyo alisema tukio hilo lilitokea katika chumba cha ofisi ya Kisuze alipokwenda kuchukua matokeo yake ya awali na barua ya uthibitisho chuoni. Wakati anavitazama hati hizo, mtuhumiwa alimkamata na kumlaza kwenye makabati ya mafaili, akamnyonya maziwa na mapaja, na kumwingiza vidole sehemu zake za siri.
Ni wakati hayo yanatokea, alitumia simu yake kupiga picha za tukio hilo na kumtishia kumshitaki ndipo mtuhumiwa alipomwachia akaondoka hapo akilia.
No comments
Post a Comment