Ripoti ya CAG yamuibua Nikki wa Pili Naye Amezungumzia
Baada ya ripoti ya (CAG) Niki wa pili mwanamziki was Hiphop nae aja na jambo lakuizungumzia hii ripoti ya (CAG)
Msanii wa Muziki wa Hip Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon maarufu kama Nikki wa Pili amefunguka kuhusu ufisadi uliotokea katika taasisi mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa, uliobuliwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na kusema kuwa kiini cha tatizo hilo ni mfumo.
Nikki wa Pili ametoa ushauri huo jana katika kongamano la mafunzo kwa umma kuhusu siasa za kiuchumi wa kitaifa ndani ya Bara la Afrika lililoandaliwa na Kavazi la Mwalimu Nyerere, yaliyoendeshwa na Mwanaharakati wa Vyama vya Ushirika kutoka nchini Afrika Kusini, Trevor Ngwane.
“Vyama vya siasa kupata hati chafu na kuiiga CCM, kwangu siyo kitu kipya sioni kama kuna tofauti kati ya vyama, mtu akitoka chama hiki anakwenda chama hiki, kimsingi mimi na weza kuwa chama A na chama hicho kikiniudhi naenda chama B na wanaipokea kwa shangwe. mnawea mkaona kwamba kuna mfanano, hizo taasisi hazitofautiani,” amesema na kuongeza.
“Tutafute mfumo ambao unarudisha madaraka mengi chini siyo juu, sababu hata vyama ukienda utakuta nguvu iko juu na wanachama wa chini hawana nguvu, tukitengeneza mfumo wa kisiasa au wa kichama ambao watu wa chini wengi watakuwa na nguvu dhidi ya sera na bajeti na kila kitu nafikiri tutaenda vyema, wanasiasa wengi ni tabaka moja na masilahi yao yanafanana.”
Na Regina Mkonde
No comments
Post a Comment