SYRIA: VIONGOZI WASHIRIKA WA RAIS ASSAD WAPANGA KUJIZATITI USITISHAJI WA MAPIGANO
Viongozi wa Uturuki, Urusi na Iran wamesema kwamba wamejizatiti katika kufikiamakubaliano ya kudumu ya usitishaji mapigano nchini Syria katika taarifa ya pamoja baadaya mkutano wa kilele ulioandaliwa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nakuwakutanisha viongozi wa mataifa hao mjini Ankara, Uturuki.
Baada ya rais Erdogan kukutana na rais wa Iran Hassan Rouhani na rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano huo wa kilele, kwa pamoja wamekubaliana nia yao ya kushirikiana kwa kile walichokieleza kama “kufikia makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano kati ya pande zinazohasimiana nchini Syria.
No comments
Post a Comment