Tunajiandaa Vipi kukabiliana Na ulimwengu wa magari ya kisasa
Mfumo wa utengenezaji magari duniani umebadilika miaka ya karibuni kutoka kwenye full mechanical kuwa advanced technology jambo ambalo ni changamoto kubwa kwa nchi zinazoendelea ambazo kwa kiasi kikubwa zinategemea magari mitumba (used).
miaka ya 90 kurudi nyuma magari mengi yalikua hayasumbui sana na spea zake zilikua simple sana kama Land rover 109, Toyota Staut,n.k
Kuna lawama kuwa gari flan mbovu , gari flan mifumo yake ya umeme ina matatizo ila ukweli ni kuwa kama gari zimeuzika sana ulaya na Asia kwa miaka 10 zina ubora ila life span yake inakaribia ukingoni! ukinunua hizi gari kama mtumba lazima likusumbue.
Gari kama hizi zinatusumbua hadi tunasema ni gari mbovu ila ukipeleka kwa Wachinna wanatengeneza maana WAO WALIJIANDAA MAPEMA.
No comments
Post a Comment