UPDATES: CHANZO CHA AJALI ILIYOTOKEA TABORA NA KUUA WATU 12 NA KUJERUHI 46 CHAELEZWA
Picha hapo juu : Ni gari aina ya Fuso Baada ya ya Kupata Ajali hiyo
Ajali ya hii imetokea majira ya saa 20:00 usiku huko kijiji cha Makomero wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora ambapo Basi lenye namba za usajili T.983 DCE mali ya Kampuni ya CITY BOY likiendeshwa na EMANUEL ATUPENDA CHITEMO mkazi likiwa linatokea Ngara Mkoa wa Kagera kuelekea Mkoa wa Dar es salaam liligongana na gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T.486 ARB lilokuwa linaendeshwa na SALUMU ABDALAH KALAMBO na kusababisha vifo vya abiria 12 huku 46 wakijeruhiwa.
Picha hapo juu: Gari kampuni ya CITY BOY mara baada ya kupata ajali.
Akiongea na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi WILBROD MUTAFUNGWA ameeleza kwamba Abiria 12 walipoteza Maisha huku wengine 46 wakijeruhiwa na kati yao aliwataja abiria watatu ambao hali zao ni mbaya na wawili wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoa wa Mwanza na mmoja Nkinga Mission wilaya ya Igunga.
Kamanda Mtafungwa ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Gari aina ya Fuso kupasuka tairi ya mbele upande wa kulia na kusababissha kukatika kwa mfumo wa usukani likiwa katika mwendo mkali baada ya kuyaingia mashimo mawili yaliyo katikati ya barabara na kusababisha kupoteza mwelekeo na kisha kuligonga basi la abiria lililokuwa likipishana nalo.
Aidha baada ya ajali hiyo dereva wa FUSO alitoweka eneo la tukio na jitihada za kumtafuta zinaendelea.
No comments
Post a Comment