WANANCHI WA IPULI KIDATO WAMPA KIPIGO MWANANCHI BAADA YA KUCHOSHWA NA MATENDO YAKE
Mkazi mmoja wa eneo la Ipuli Kidato Tabora Mjini aliefahamika kwa jina la Saidi Ramadhani amechezea kichapo cha Tumekuchoka (Mbwa mwizi) kutoka kwa wananchi wa Mtaa huo kwa kile ninachodaiwa ni kuchoshwa na tabia yake ya wizi na ukabaji uliokithiri
Tukio hilo limetokea jana Jumapili ya 29April majira ya saa1 jioni baada ya kutokea tukio la wizi katika nyumba moja (jina linahifadhiwa kwa sababu maalumu) maeneo hayohayo ya Kidato, Ndipo wananzengo walipiga ramli na kumshakia Bwana Said kua ndie aliefanya uhalifu huu hakuna mwingine
Wananchi walijikusanya kwa lengo la kufanya uvamizi kwa mtuhumiwa wao,kwa mujibu wa mnyetishaji amesema kua wananzego baada ya kukubaliana na kuthibitisha utabili wao kuwa bwana Said ndiye muhusika wa wizi uliofanyika, Walivamia nyumbani kwake na kufanikiwa kumkuta akiwa mwenye furaha ya kufurahia ushindi wa wizi alioufanya
Wananzego hawakutaka kufungua mahakama ya mwanzo wala ya rufaa kwa kutaka kumuhoji mtuhumiwa wao kama amehusika au laa, Walianza kutoa adhabu waliyohisi inaendana na makosa aliyoyafanya kwa kumpa kichapo cha Tumekuchoka kwa kutumia silaha za jadi
Polisi walifanikiwa kutonywa juu ya Mahakama hiyo iliyofunguliwa mtaani na wananzengo Polisi waliwahi kufika eneo la tukio na kuondoka na mtuhumiwa huyo hali iyozua minong'ono kwa wananzengo wakimlaumu mtu alietoa taarifa kwa Polisi angeacha kidogo
No comments
Post a Comment