Followers

Zaidi ya Shule Ishirini Zachomwa Moto Kwenye Mapigano DR Congo




Takriban shule ishirini zimechomwa moto kutokana na mapigano yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa mujibu wa habari,ndani ya wiki mbili zilizopita shule za msingi na sekondari zimekuwazikiangamizwa kwa moto katika mapigano ya kikabila kaskazini mashariki mwa DRC.
Afisa polisi Ivan Legu amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa zaidi ya shule 60 zimefungwa katika vijiji sita eneo la  Djugu,Ituri.
Hii ni kutokana na mapigano na mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa kati ya jamiiza Lendu na Hema.
Zaidi ya watu arobaini wamepoteza maisha katika mapigano hayo,hali iliyoilazimu serikalikutuma majeshi kutuliza ghasia lakini bado haikusaidia.
Eneo la Ituri linaongoz katika mapigano ya kikabila na kusababisha vifo vya wengi.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.