ZITTO KABWE:SERIKALI INASEMA UONGO,NI MUHIMU BUNGE LICHUNGUZE ZILIKO TRILIONI 1.5
DODOMA. Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini mkoani Kigoma, amesema serikali imesema uongo katika ufafanuzi wa upotevu wa fedha za kitanzania kiasi cha trilioni moja nukta tano(1.5) zilizooneka kutumika bila kuidhinishwa na bunge katika matumizi ya fedha ya mwaka 2016/2017 kama ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu ilivyoainisha.
Zitto amesema hayo katika taarifa ya ACT-Wazalendo ya leo April 20,2018, baada ya majibu ya serikali bungeni yalitolewa leo na Naibu waziri wa fedha, Dkt Ashatu Kijaji, kuhusu Ziliko fedha Tril 1.5 zisizoonekana matumizi yake kwenye ripoti ya CAG.
Amesema kuwa maelezo hayo ni yale yale, aliyoyatoa Katibu mwenezi taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu mwenezi taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu. Na kudai kuwa taarifa ya serikali ya leo na taarifa ya fedha ya benki kuu zinakinzana.
“Tutaongea na waandishi kueleza hili kwa undani zaidi. Ijulikane tu kuwa akaunti za serikali kwenye taarifa za fedha za benki kuu hazina hizo fedha Naibu waziri ametaja.
“Ni dhahiri kuwa kuwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, ndio maana taharuki ya serikali ni kubwa, kiasi cha majibu ya serikali kupewa kiongozi wa CCM kuyasema, na kwa kuwa kashindwa kukonga nyoyo, sasa imebidi Serikali ije yenyewe kuyasema majibu yale yale yaliyosemwa na CCM.” Amesema Zitto.
Mhe. Zitto ameshangaa kwani ameshuhudia kwa mara ya kwanza, Zanzibar ikikusanyiwa zaidi ya TZS bilioni 200 Sawa na 20% ya bajeti nzima ya Zanzibar, makusanyo yote ya TRA Zanzibar na mara 10 zaidi ya makusanyo ya Zanzibar kutoka PAYE za muungano ambazo ndio pekee hukusanywa na TRA.
“Uongo huu wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), lazima unasukumwa na wizi. Zanzibar hukusanyiwa TZS bilioni 21 tu na TRA, bilioni 200 zinatoka wapi? Balaa.” Aliuliza mhe Zitto.
Aidha, mbunge huyo alimaarufu ZZK, amemsihi pika wa bunge kuruhusu ukaguzi maalumu wa matumizi ya shilingi 1.5 trilioni, kupitia kamati ya bunge ya hesabu za serikali(PAC), kwa kudai kuwa kiutaratibu majibu ya serikali yanapaswa kuhakikiwa kwanza na CAG kabla ya kusomwa bungeni, jambo ambalo halikufanyika.
“PAC wanajua kuwa makusanyo ya Serikali ni cash basis na sio accrual. Serikali imedanganya, lazima PAC sasa wafanye kazi yao. Muhimu; tamko la serikali ni matusi Kwa CAG. Watanzania mjiandae kuilinda taasisi ya ukaguzi wa taifa. Serikali ya CCM inataka kuivunja vunja taasisi hii ya uwajibikaji. Tusikubali.” Amesema Zitto
No comments
Post a Comment