Burundi yapiga marufuku matangazo ya BBC na VOA
Serikali ya Burundi inasema matangazo ya mashirika ya utangazaji ya BBC na VOA yamepigwa marufuku nchini humo kwa miezi sita kuanzia Mei 7 mwaka huu kwa, 'kutofuata sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini' na 'kukiuka maadili ya kikazi'.
Inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.
Hatahivyo waandishi wa habari wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida nchini humo.
Matangazo ya BBC hupeperusha nchini Burundi kupitia masafa ya FM na kwa kupitia radio mbili washirika.
BBC inajitahidi kuwasiliana na serikali ya Burundi kuhusu uamuzi huo.
- Kampeni za kura ya maoni zimeanza rasmi nchini Burundi
- Wakimbizi wa Burundi waanza kurejea kutoka Tanzania
Mtandao wa habari nchini humo umetuma nyaraka ya taarifa hiyo
Nchi hiyo inajitayarisha kwa kura ya maoni Mei 17 ambayo huenda ikamuongezea muda wa kuhudumu rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch linasema vikosi vya serikali ya Burundi na wafuasi wa chama tawala wamewaua , kuwapiga na kuwatesa watu wanaowaona kama wapinzani wa kura hiyo ya maoni.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani hivi karibuni imesema huenda kura hiyo ikaathiri taasisi za demokrasia nchini humo.
Radio kadhaa za kibinfasi zimeharibiwa na kufungwa nchni humo wakati wa mzozo wa kisiasa ulioanza mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza aliposhinda muhula wa tatu madrakani, uliozusha mzozo.
Tangu hapo, takriban watu 430,000 people, wakiwemo wanasiasa wa upinzani wameitoroka Burundi.
No comments
Post a Comment