Followers

Guterres amuonya Trump kuhusu Iran

The new secretary-general of the UN, Antonio GuterresHaki miliki ya pichaAFP
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka Marekani kutojiondoa kutoka katika mkataba wa kimataifa uliopangwa kudhibiti uwezo wa nyuklia ya Iran.
Akizungumza na BBC ameonya kwamba kuna hatari ya vita iwapo makubaliano hayo hayata tunzwa.
Guterres amesema makubaliano ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu hayapaswi kutelekezwa isipokuwa kuwe na mbadala mwingine mzuri zaidi.
Viongozi wa Ulaya wamemtaka pia Rais Donald Trump wa Marekani kubakia katika makubaliano hayo.
Rais huyo wa Marekani aliyaita makubaliano hayo kwamba ni mkataba mbaya zaidi na kuonesha nia ya kutaka kujitoa.
Anatarajia kutoa uamuzi wake katika siku chache zijazo.

PAKUA[DOWNLOAD] SASA APPLICATION YA SUPERNIDA KUPATA HABARI ZOTE KILA SAA BONYEZA HAPA >>>>DOWNLOAD SASA BONYEZA HAPA.>>>>>

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.