Followers

Magufuli: Si wanafunzi wote wa vyuo vikuu watakaopewa mikopo Tanzania

Rais MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya nchi hiyo haiwezi kutoa mikopo ya kimasomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini humo.
Kiongozi huyo alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.
"Nataka niwahakikishie Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini lazima niwaambie ukweli Serikali haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote" alisema.
Dkt Magufuli alisema hayo alipokutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo katika Manispaa ya Iringa ambapo alisikiliza kero zao mbalimbali zikiwemo zinazohusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na mazingira ya kusomea, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Rais Magufuli alisema utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ni lazima ufuate taratibu pamoja na historia ya familia.
Alidokeza kwamba watakaopewa kipaumbele ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na uhandisi.
"Hili suala la mikopo lina changamoto, ndiyo maana tunapotoa mikopo tunaangalia historia ya mtu, ndiyo maana mtoto wangu hapati mkopo," alisema kwa mujibu wa gazeti la kibinafsi la Mwananchi.
Takwimu za mikopo Tanzania
"Huwezi kumsomesha mtoto shule ya msingi ya binafsi, halafu baadaye aje aombe mkopo. Hao waliokusomesha wapo wapi? Na kama hawapo tutataka uambatanishe nyaraka kuonyesha hawapo."
Rais huyo alitania kwamba wanawe walijaribu kutumia ujanja wa kutumia jina la mama yao kupata mikopo lakini hawakufanikiwa.
"Hawa majamaa wajanja sana, tulijaribu kutumia jina la mama yao lakini bado wakawagundua," alisema.
Mwishoni mwa mwaka jana, serikali ya Tanzania iliidhinisha Sh427 bilioni za mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18, lakini viongozi wa wanafunzi walilalamika kuwa bajeti hiyo ilikuwa ndogo ukilinganisha na mahitaji.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya viongozi wa wanafunzi walisema bajeti hiyo imekuwa ikizidi kupungua licha ya wanafunzi kuongezeka.
Faraja Nyarandu
Mkurugenzi wa haki za wanafunzi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo aliambia gazeti la Mwananchi wakati huo kwamba bajeti hiyo imekuwa ikizidi kupungua licha ya wanafunzi kuongezeka.
Mwaka 2016/17 serikali ilitenga Sh483 bilioni kwa wanafunzi 120,000 za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
"Cha kushangaza mwaka wa masomo 2017/18 wanafunzi wameongezeka na kufikia 122,000, lakini badala ya fedha za mkopo kuongezeka zimepungua na kuwa Sh427 bilioni waombaji wakiwa 61,000 na Serikali imesema itawapa 30,000 pekee," alisema.
Lakini naibu waziri wa Elimu, William Ole Nasha alisema Serikali imetenga fedha hizo kulingana na maombi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Alisema: "Kuna vigezo ambavyo vimewekwa na kulingana na vigezo hivyo bodi imejiridhisha fedha hizo zinatosha, bodi ingeomba halafu Serikali ingepunguza lawama hizo zingekuwa na tija."
Alieleza kuwa vigezo vinavyotumika ni ngumu kubaini ukweli wake kwa sababu si kila anayeishi katika familia bora ana uwezo.
Magufuli akikagua ujenzi wa ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa mkoani IringaHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionMagufuli akikagua ujenzi wa ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa mkoani Iringa
Mkurugenzi wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema changamoto iliyopo ni baadhi ya wanafunzi na wazazi kuamini hata kama wana uwezo ni lazima wapate mkopo.
"Siyo kweli kwamba wanafunzi Tanzania nzima hawana uwezo wa kumudu gharama za kusoma vyuoni, ila imejengeka dhana kuwa wakifika chuo kikuu lazima walipiwe na Serikali," alisema.
Miongoni mwa changamoto zinazokabili mpango wa utoaji mikopo kwa wanafunzi Tanzania, kwa mujibu wa serikali, ni baadhi ya wanafunzi walionufaika kutolipa pesa hizo.
Mapema mwaka huu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wiki ijayo ilitangaza kuanza kuwasaka jumla ya wanufaika 119,497 nchini kote ambao wamekiuka sheria iliyoanzisha Bodi hiyo.
Wanufaika hao walidaiwa kutoanza kurejesha mikopo yenye thamani ya TZS 285 bilioni waliyokopeshwa tangu mwaka 1994/1995 na mikopo yao

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.