Followers

Manara afunguka sakata la kuihama Simba




Afisa Habari wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai sio kweli ana mpango wa kutaka kuikacha Klabu yake ya wekundu wa Msimbazi na kuitaka jamii kuzipuuza taarifa hizo pindi watakapokutana nazo au kusikia.

Manara amebainisha hayo mchana wa leo Mei 02, 2018 kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo na taharuki kubwa kwa wapenzi wa soka kutokana na kusikia taarifa zinazomuhisha kiongozi huyo kutaka kuikimbia Simba bila ya kuwepo na sababu maalum juu ya jambo hilo.

"Siondoki Simba na naomba muelewe hivyo, ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi. Rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hivyo, walichokitangaza ni uzushi nawezaje kuwaacha simba kipindi hiki muhimu", amesema Manara.

Jibu hilo la Manara limeweza kurudisha furaha na bashasha kwa wapenzi wa klabu ya Simba kwa kile wanachokiamini kuwa kiongozi huyo anawapa hamasa nyingi wakati wa kuelekea mchezo hata baada ya matokeo vile vile.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.