Mkwawa adakwa na Jeshi la Polisi
JESHI la Polisi mkoani Iringa linamshikilia aliyekuwa MKuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), Profesa Philemoni Mushi (65), mkazi wa Makongo Juu, Dar es Salaam.
Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire, alisema Profesa Mushi alikamatwa juzi majira ya saa sita mchana baada ya kupewa wito wa kipolisi.
Kamanda Bwire alisema Prof. Mushi bado anaendelea na kazi kwa muda za kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Alisema kwa sasa anaendelea kuhojiwa na baada ya mahojiano atafikishwa mahakamani, ili sheria ichukue mkondo wake.
Kukamatwa kwke Prof. Mushi kunatokana na amri ya Rais John Magufuli kutaka akamatwe kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa ukumbi wa chuo hicho chini ya kiwango.
No comments
Post a Comment