Pango walilojificha Wajerumani wakati wa vita lagunduliwa Mtwara.
TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA SUPERNIDA BLOG,KWA MAWASILIANO ZAIDI TUPIGIE SIMU 0767673288AU 0675830390
Maafisa wa Taasisi ya kimataifa ya Trade Aid kwa kushirikiana na wazee wa mji wa Mikindani wamebaini pango la ajabu kwenye jiwe, Pwani ya Bahari ya Hindi linaloitwa Nyumba ya Mungu lililotumiwa na Wajerumani kujificha wakati wa vita vya pili vya dunia, ambapo wameiomba serikali kusaidia kuhifadhi eneo hilo, kama sehemu muhimu ya kuvutia watalii.
Wakizungumza na ITV wazee hao wenye umri wa miaka kati ya 90 na 95 wamesema pango hilo lenye vyumba kadhaa,wanaliita nyumba ya mungu kwa kuwa hakuna binaadamu aliyelichonga, na kwa sasa baadhi ya wakazi wa Mikindani na maeneo mengine wanalitumia kufanyia matambiko kama kuomba mvua au usalama.
Aidha wamebaini pia makaburi walikozikwa watu warefu, wenye urefu kati ya futi nane na futi 10 eneo la Kiseti Kyanga katika karne ya 18.
Wakizungumzia matukio hayo, Mwakilishi wa Taasisi ya Trade Aid nchini Emmanuel Mwambe amesema maeneo hayo mawili yanafaa kutunzwa kama sehemu ya kuvutia watalii, huku Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha STAMCO Mtaalamu wa historia Daktari Festo Gabriel amesema hiyo ni ishara ya kuonyesha mkoa wa Mtwara una utajiri mkubwa wa mambo ya kale na hivyo ameiomba serikali kuelekeza jicho lake kwenye matukio hayo kwa kuwa historia ni urithi na pia uchumi.
No comments
Post a Comment