Tahadhari Imetolewa Iringa kwa wafuasi wa CHADEMA; Rais Magufuli
Mchungaji Peter Msigwa na Rais Magufuli (kulia kwenye picha) |
Mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Mhe. Peter Msigwa amewakaribisha wageni wote mkoani humo akiwemo Rais Magufuli katika kusherehekea siku ya Mei Mosi na kuwaomba wanachama wa CHADEMA na wafuasi wa UKAWA wasivae jezi za vyama kwenye sherehe hizo.
Mchungaji Msigwa kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Mei 1, 2018 amesema kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaichukulia siku ya wafanyakazi duniani kama sehemu ya kufanya siasa kwenye majukwaa, kitu ambacho kimepelekea bendera za CHADEMA kung’olewa kwenye nguzo na kuwekwa bendera za CCM.
“Wenzetu wanatumia sherehe hizi kisiasa kwa kung’oa bendera za chadema na kuweka bendera za CCM hata kwenye nguzo za umeme! Kinyume cha utaratibu, Utadhani ni sherehe ya kuzaliwa kwa CCM. Mji ungepambwa kwa bendera za taifa ingeleta mshikamano na umoja wa Taifa. Kwa bahati mbaya wameahindwa kuona hili.“amesema Msigwa na kutoa tahadhari kwa wafuasi wa CHADEMA na UKAWA.
Hata hivyo niwaase wapenzi na wanachama wa CHADEMA na UKAWA! Wasije uwanjani na nembo au bendera za vyama .Tuonyeshe ukomavu na uelewa wa kisiasa. Michelle Obama aliwahi kusema “when they go low we go high”. Niwaombe tuwakarimu wageni wetu watamani kurudi Iringa tena na tena. Ili tukuze uchumi wa Manispaa yetu.”amesema Msigwa.
Leo Mei 01, 2018 ni siku ya wafanyakazi duniani na maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yanafanyika mkoani Iringa na mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
No comments
Post a Comment