Followers

UPUNGUFU WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME (LOW SPERM COUNT)



Image result for spermatogenesis


Upungufu katika uzalishaji wa mbegu za kiume inahusiana na kutokuwepo kwa mbegu za kiume kwenye manii au uwepo wa mbegu kidogo sana katika manii.
Mbegu za kiume huwa zinachunguzwa kwa kutumia kifaa maalum au darubini katika
maabara, kwa kawaida mwanaume ili aweze kumpa mwanamke mimba anatakiwa atoe kiasi cha mbegu kati ya milioni ishirini hadi milioni mia nne kwa tendo, chini ya milioni ishirini huwezi kumpa mimba mwanamke.
Endapo kiwango cha mbegu zitakuwa kidogo kitaalam hali hiyo huitwa ‘Oligospermia’ na kama huna kabisa mbegu hali hiyo huitwa
‘Azoospermia.Dalili za kutokuwa na mbegu za kiume Hakuna dalili za moja kwa moja kusema kwamba utaumwa kitu fulani, lakini dalili
zifuatazo huambatana na tatizo hili;
=kwanza ni kukaa katika mahusiano kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja lakini mwenzi wako hapati mimba, =kushindwa kufanya
tendo la ndoa kwa uume kukosa nguvu’ Low
sex Drive’ na
=ukisimama unashindwa
kuendelea na kumalizia tendo ‘Erectile dysfunction’ pamoja na kuwahi kumaliza tendo la ndoa.
=Maumivu na uvimbe wa korodani, =kupungua kwa vinyweleo na ndevu kutoota pia ni dalili inayoashiria matatizo ya uzazi kwa mwanaume kwani ni ishara ya upungufu wa
Kromozomu au homoni za kiume.
Hizo zote ni dalili kuu za matatizo ya uzazi kwa mwanaume.
Kipindi au Wakati gani wa kumuona daktari au mtaalamu?
Endapo umekaa na mwenzio mwaka mmoja au zaidi, mnafanya tendo la ndoa bila kinga yaani kizuizi chochote wakati wa kupangilia ujauzito lakini mimba haipatikani. Kama una matatizo ya nguvu za
kiume au unawahi kumaliza tendo la ndoa. Unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au uume unalegea wakati wa tendo pia ni mojawapo ya chanzo.
Unakuwa na maumivu ya korodani au korodani kuvimba, maumivu ya uume na maumivu wakati wa kukojoa au uwepo wa kivimbe katika uume.
Chanzo cha tatizo Uzalishaji wa mbegu za kiume unafuatana
na ubora wa korodani kama haina tatizo lolote na kiwango bora cha mfumo wa homoni mwilini mwako. Homoni zinadhibitiwa katika ubongo na kuimarisha korodani zizalishe mbegu. Mbegu zikishazalishwa,
husafirishwa na mirija midogo sana na laini hadi katika tezi dume ’Prostate gland’ ambayo kazi yake kubwa ni kuzalisha manii. Matatizo katika mbengu za kiume ni kutokuwepo kwa mbegu kunakosababishwa na hitilafu au matatizo kwenye korodani, kuzalisha mbegu zenye kasoro, mbegu zisizo na kiasi na mbegu chache.
Matatizo ya korodani husababishwa na joto kali katika korodani, maambukizi katika korodani na uume na kuumia korodani. Mishipa ya damu kulalia korodani ‘Variocele’ pia ni mojawapo ya tatizo kubwa la kuziba
kwa mirija ya usafirishaji mbegu hizo.
Zipo pia sababu za kimazingira zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume mfano kemikali za viwandani, rangi za viwandani
au majumbani, dawa za mashambani na za kuua wadudu, mionzi ya X- Ray, kukaa kwenye joto kali, kuvaa nguo za kubana na
kukaa mahali kwa muda mrefu, kupakata kompyuta ‘(Lap top)’ kwa muda mrefu, matumizi ya sigara, bangi na madawa mengine ya kulevya kwa muda mrefu na
ulevi uliokithiri. Uzito mkubwa wa mwili na matatizo ya akili.
Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia mwenendo wa mfumo wa homoni mwilini Kipimo cha Ultrasound kuangalia korodani yako kwa
ndani. Uchunguzi hufanyika kisayansi hospitali tu, hakuna vifaa vingine vya kuchunguza kwa
kubahatisha, unatakiwa utolewe damu, na utoe mbengu zako za kiume baada ya kupumzika kufanya tendo la ndoa angalau
kwa siku tatu.
Matibabu na ushauri hufanyika baada ya uchunguzi ambapo
daktari atatoa dawa kuzingatia na tatizo lililopo. Kama hakuna mbegu zipo chache au kuna maumivu au kasoro zozote. Uwepo wa kasoro
za viungo vya uzazi pia ni tatizo mfano, uume mfupi, kutokuwa na korodani au kuwa na korodani moja.
Upande wingine wanaume anaweza kuwa anazalisha mbegu za kutosha lakini anashindwa kumpa mweza wake ujauzito kutokana na matatizo aliyonayo mwenza wake kama
=kuwa na acidic katika uzazi ambapo huuwa mbegu za kiume zikifika ndani ya kizazi
=kuzalisha yai ambalo halijakomaa kwa wanamke
=kuhalibika kwa kuta za kizazi 'uterus' au kuwa zaifu na kushindwa kuhimili au kubeba ujauzito.
=upande mwingine wanaume kuzalisha mbegu mbovu au zenye matatizo.
Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea page zetu Facebook kwa jina la *afya kwa wanaume* na *afya ya wanawake* pia unaweza kiwasiliana nasi kwa ushauri na tiba ya uhakika.
Piga namba hizi 0767421678 au 0655148030.
SHARE NA LIKE ELIMU HII IWAFIKIE WENGINE ILI WAJIFUNZE NA KUELIMIKA ILI KUPUNGUZA MATATIZO YA UZAZI NDANI YA JAMII ZETU.

PAKUA[DOWNLOAD] SASA APPLICATION YA SUPERNIDA KUPATA HABARI ZOTE KILA SAA BONYEZA HAPA >>>>DOWNLOAD SASA BONYEZA HAPA.>>>>>

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.