Followers

FAIDA 9 ZA MAJANI YA MPERANA PERA


                            
Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla
Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium.
Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike,
Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika.

Jinsi ya kuyatengeneza kama dawa
Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.
Ukimaliza fanyia masaji nywele zako kama mtu anayepaka mafuta nywele zote.
Baada ya hapo unaweza kuacha kwa muda kama steaming kisha ukaosha.
Fanya hivi mara kwa mara, walau mara 3 kwa juma, naamini utaona mabadiliko.

FAIDA PIA ZA MATUNDA YAKE (MAPERA YENYEWE)
Mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C pamoja na vitamin A na inaelezwa kuwa kiwango cha vitamin C kinachopatikana ndani ya pera ni mara nne ya kiwango cha vitamin hiyo kinachopatikana kwenye chungwa.
Pia mapera yamesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin B2, E na K pamoja na madini ya chuma, ‘copper’, ‘potassium’ na ‘manganese.’
Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa na Jarida la Journal of Human Hypertension mwaka 1993 ulieleza kuwa tunda aina ya pera hupunguza kiwango cha msukumo mkubwa wa damu ndani ya mwili yaani ‘High Blood Pressure’ hii ni kwa sababu ya madini ya potassium na vitamin C ambayo husaidia kuweka sawa msukumo wa damu ndani ya mwili.
1. Utajiri wa Vitamin C:
Mapera yana utajiri mkubwa wa Vitamin C ambayo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu.
2. Ni kinga nzuri ya kisukari.
Ulaji wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari Hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa Fibre.
Fibre ni muhimu sana katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Vilevile ni muhimu sana katika kuusafisha mfumo wa usagaji
3. Kuimarisha Uwezo Wa Kuona
Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri.
Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera yanasaidia sana katika kuongeza na kuimarisha uwezo wa mtu kuona.
4. Kusaidia katika Uzazi
Mapera yana madini yaitwayo Folate ambayo husaidia katika kurutubisha mayai ya uzazi..
5. Kurekebisha Kiwango Cha Shinikizo la Damu
Madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera yanasaidia katika ku-normalise shinikizo la damu (Blood Pressure)
Ndizi na mapera vina kiwango cha potassium sawa.
6. Utajiri mkubwa wa Madini Ya Shaba
Mapera yana madini ya shaba (Trace element copper) ambayo ni mazuri sana katika ku- maintain ufanyaji kazi wa tezi ziitwazo thyroid.
Tezi za thyroid zisipofanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya kwa mwanadamu.
7. Utajiri wa Madini Ya Manganese
Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya manganese ambayo yanausaidia mwili katika kunyonya ama kupata virutubisho muhimu kutoka kwenye vyakula tunavyo kula.
Chakula tunachotumia kikitumika vizuri mwilini, tunapata virutubisho vyote muhimu kama vile biotini, vitamin nakadhalika
8. Kuusadia mwili na akili katika ku–relax
Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya magnesium ambayo hufanya kazi ya kuvifanya akili na mwili wa mwanadamu viweze ku relax. Unashauriwa kutumia mapera baada ya kazi nzito. Hii itasaidia katika kuufanya mwili na akili yako kupumzika
9. Mapera ni muhimu katika afya ya akili ya mwanadamu.
Vitamin B3, Vitamin B6 ambazo zinapatikana ndani ya tunda la mpera muhimu katika kuimarisha afya ya akili

Ukiitaji dawa au ushauri
Dr Hamza
0654729438
0746025804

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.