Followers

Kesi ya Mbowe na wenzake yaendelea, pingamizi latupiliwa mbali

Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa ulahisi zaidi Bonyeza Hapa


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali pingamizi la viongozi wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe la kutaka kesi ya kufanya maandamano ifutwe badala yake imeagiza hati ya mashtaka ibadilishwe.

Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia wakili wa Peter Kibatala, umetangaza nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema anakubaliana na hoja 2 za upande wa mashtaka kati ya hoja zao 8 za pingamizi.

Katika kesi hiyo pingamizi kuu la upande wa utetezi wameiomba mahakama hiyo ifute kesi hiyo kwa sababu baadhi ya mashtaka ni batili.

Katika uamuzi wake Hakimu Mashauri amesema hakuna haja ya kesi hiyo kufutwa badala yake anaagiza upande wa mashtaka uifanyie marekebisho hati ya mashtaka.

Hata hivyo, wakili Kibatala amedai kuwa wanatangaza nia ya kukata rufaa kwa sababu kama mahakama imeona mashtaka hayo ni batili kwanini isingeyafuta badala yake imeagiza yabadilishwe.

Upande wa mashtaka kupitia Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi umedai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mahakama za Mahakimu hakuna uwezekano wa kukata rufaa katika uamuzi mdogo ambao hauwezi kuathiri kesi.

“Naomba mahakama ipuuzie hoja hizo na nia hiyo ni batili,”ameeleza Kadush
Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa ulahisi zaidi Bonyeza Hapa

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.