Maisha ya Yanga kabla na baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji
TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA SUPERNIDA BLOG,KWA MAWASILIANO ZAIDI TUPIGIE SIMU 0767673288AU 0675830390
Kwenye kipindi cha Sports Xtra cha Leo kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga alizungumza mambo mengi yanayohusu klabu hiyo.
Miongoni mwa mambo ambayo aliyadadavua upana ni maisha ya Yanga kabla na baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.
“Tunashukuru kwa alichofanya Manji katika kipindi chote ambacho alikuwa madarakani na kabla ya kuwa madarakani wakati huo akiwa mdhamini wa klabu, amekuwa ni msaada mkubwa.
Kila mwanachama na mpenzi wa Yanga anajua maisha tuliyokuwa nayo wakati huo, Manji alikuwa mpiganaji na timu iliweza kufanya vizuri kwa kipindi chote ambacho alikuwepo.
“Katika kipindi cha hivi karibuni wakati Manji yupo Yanga tuliweza kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kambi mbalimbali hakukuwa na tatizo la kulipa mishara, ilikuwa inalipwa kwa wakati.
Aina ya wachezaji na benchi la ufundi lilikuwa ni zuri sana katika vipindi vyote ambavyo alikuwepo na hakukuwa na dosari.” **Amesema Clement Sanga katika #SportXtra.
No comments
Post a Comment