Atiwa mbaroni baada ya kukutwa na kilo 80 za bangi
DOWLOAD APP YA SUPERNIDA BLOG KWENYE SIMU YAKO ILI KUPATA HABARI ZETU ZOTE KWA HARAKA NA RAHISI ZAIDI, BONYEZA HAPA
Akizungumzia hilo leo Julai 10, Kamanda wa polisi Mkoani Shinyanga, Simon Haule amesema mtuhumiwa huyo, amekamatwa jana saa 7, mchana eneo la daraja la Manonga kijiji cha Isaka, wilaya ya kipolisi ya Msalala, Shinyanga.
Amesema mtuhumiwa huyo alitumia mbinu ya kuchanganya bangi na mizigo mingine ya pamba aliyokuwa amebeba kwenye gari hilo ili asibainike.
“Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kufanikiwa kukamata gari hilo na baada ya kulipekua walikuta magunia hayo ya dawa za kulevya aina ya bangi,”amesema Haule
Kamanda Haule amesema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Hata hivyo, Haule ametumia muda huo kukemea vitendo vya baadhi ya wananchi kujihusisha na biashara haramu ya bangi ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu na yanadhoofisha jitihada za serikali za kukuza uchumi.
No comments
Post a Comment