Costech wailima barua TWAWEZA Kwa Kutoa Utafiti Bila Kibali
DOWLOAD APP YA SUPERNIDA BLOG KWENYE SIMU YAKO ILI KUPATA HABARI ZETU ZOTE KWA HARAKA NA RAHISI ZAIDI, BONYEZA HAPA
Tume ya Sayansi na Teknolojia (Comstech) imeiandikia taasisi barua na kuitaka ieleze ni kwa nini haifai kuchukuliwa hatua za kisheria.
Barua hiyo inasema Twaweza waliwasilisha maombi ya vibali vya kufanya utafiti awali nchini Tanzania lakini utafiti huo wa Sauti ya Wananchi haukujumuishwa.
"Mwishoni mwa wiki kulikuwa na taarifa kuhusu utafiti mpya wa Twaweza kwa jina Sauti za Wananchi.
Kwa kuwa tume hii haina rekodi zozote kwamba ilitoa kibali kwa Twaweza au kuna ombi la kibali cha utafiti kama huo ambacho kiliwasilishwa, kuchapishwa kwa matokeo ya utafiti huo kunakiuka kifungu 11 cha Mwongozo wa Kusajiliwa na Kuidhinishwa kwa Usajili wa Kitaifa kwa kutoandikisha mradi huu wa utafiti kwa Soctech."
Twaweza wamethibitisha kwamba wameipokea barua hiyo lakini bado hawajatoa tamko rasmi.
Utafiti huo wa Twaweza ulikuwa unasema asilimia 65 ya wananchi Watanzania walisema hawako tayari kutumia njia ya maandamano kuishinikiza serikali katika mambo yasiyowaridhisha.
Kwa upande mwingine, mwananchi mmoja kati ya wanne (27%) ana uwezekano wa kushiriki kwenye maandamano.
Ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2016, idadi ya wanaosema wana uwezekano wa kushiriki ilishuka kidogo sana (kutoka 29% mpaka 27%) wakati ambao wanasema hawana uwezekano wa kushiriki imeongezeka (kutoka 50% mpaka 65%).
Wananchi wachache kwa hiari walitaja maandamano kama njia ya kufikisha malalamiko yao kwa serikali. Idadi kubwa ya wananchi walisema hawako tayari kushiriki kwenye maandamano kuhusu jambo lolote lisilowapendeza.- ikiwemo idadi kubwa ya wafuasi wa vyama vya upinzani.
Na wananchi wengi zaidi wanaunga mkono serikali kukataza mikutano na maandamano ya kisiasa kuliko wale wanaopinga.
Utafiti wa Twaweza ulitaja sababu kadhaa za kutofanyika maandamano ya tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 2018 kama yalivyokuwa yamepangwa na mwanaharakati Mange Kimambi.
Utafiti huo pia ulibaini kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeshuka kutoka asilimia 96 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 55 mwaka huu.
Asilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016, na 71% mwaka 2017.
Mange Kimambi: Mwanaharakati mwiba kwa serikali ya Magufuli
Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.
Msemaji na katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwana Humphery PolePole alikosoa utafiti huo wa Rais Magufuli bado ni maarufu sana nchini Tanzania kutoka na sera zake.

No comments
Post a Comment