Followers

Hizi ndizo sababu za kutoweza kufanikiwa kwako


Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa urahisi zaidi Bonyeza Hapa

U hali gani mpenzi msomaji wa Muuungwana blog bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majumu yako ya kila siku, naomba siku ya leo niweze kusema na wewe sababu za wewe kuendelea kuwa maskini.

Sababu hizo ni:

1. Kutokuwa na vipaumbele.
Ama hakika maisha ni vipaumbele hii ni kwa wale tu, ambao wana uelewa timamu, hii ni kwa sababu mtu asipokuwa na vipaumbele atakuwa ni mtu wa kufanya vitu ambavyo havina maana yeyote ile katika maisha yake.

Kwa hakika kuna vitu vingi vya kufanya kwa siku. Lakini ili uweze kuvikamilisha vyema huna budi kuweka mpangilio mzuri kwa kutegemea umuhimu kwa kila kitu.

Kuwa na vipaumbele kutakuwezesha kufahamu ni kazi ipi ianze na ifanyike kwa muda gani badala ya kufanya lolote linalokuja mbele yako.

2. Marafiki.
Inawezekana unafanya kazi kwenye ofisi au katika eneo ambalo umezungukwa na marafiki zako. Kwa njia moja au nyingine wafanyakazi wenzako au marafiki zako wanaweza kukuzuia kukamilisha kazi zako.

Kwa mfano ukiwa uko ofisini na ukaanza mazungumzo na mfanyakazi mwenzako, ni wazi kuwa utapoteza muda mwingi wa kazi.

Inawezekana pia una rafiki anayekushawishi kufanya mambo kama vile kumsindikiza kwenye matembezi au kukuingiza kwenye mazungumzo na shughuli nyingine ambazo hazihusiani na kazi zako.

Moja kwa moja unaona jinsi ambavyo unaweza kupoteza muda mwingi ambao ungeweza kuutumia kukamilisha kazi zako.

Hivyo kila wakati epuka sana marafiki ambao hawana mchano wowote katika maisha yako.
Mwisho kabisa Muungwana Blog inakutakia siku njema na mafanikio mema pia.

Install Application hii ya supernida ili Upate Habari Kwa urahisi zaidi Bonyeza Hapa

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.