Followers

Lugola aeleza sababu zilizompelekea kuvunja Baraza la Usalama Barabarani

 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola amebainisha kwamba sababu kuu zilizompelekea yeye kuvunja Baraza la Usalama wa Barabarani Taifa hadi kwenye ngazi ya mikoa hadi wilaya siku ya jana ni kutokana na kutaka matokeo chanya ya haraka ili rais pia aweze kupumzika.

Mh. Lugola amefunguka hayo leo wakati akizungumza na East Africa Radio katika kipindi cha East Africa Breakfast ambapo ameeleza kwamba Rais aliamua kumteua kwenye nafasi hiyo kwa kumuamini na yeye ameamua kuchukua maamuzi hayo kisheria kwa kuwa anataka Rais aendelee kuwatumikia wananchi kwenye sehemu zingine na siyo kushughulika na ajali.

Lugola amesema alifikia uamuzi wa kuvunja Mabaraza  baada ya kujiridhisha kupitia Wajumbe wa kwenye mabaraza hayo ya Usalama  na kugundua kuna mapungufu mengi ikiwepo kutofuata sheria, kutozijua sheria na na hawana uwezo ilhali wapo kwenye idara hizi kwa takribani miaka 10.

Aidha kiongozi huyo ameeleza kuwa  "Hatua nilizochukua ni za kisheria kabisa na nimekuwa kwenye jeshi kwa muda mrefu sana nikilitumikia, najua kulikuwa na uzembe katika kuzitekeleza sheria na ndiyo maana mimi nilipoingia nimeanza sheria" Nataka Rais wangu apumzike na kutuma salamu za rambirambi. Nikiwa kama Waziri ninayetaka matokeo chanya lzima nifanye sheria inavyotaka" Lugola.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.