Mbinu 3 Za Kugundua Fursa Za Kibiashara Mahali Ulipo
Kila kitu ambacho unakiona mbele ya macho yako ni lazima ukitafakari katika ubongo usiokuwa wa kawaida, yaani ni lazima uwaze kitakupaje pesa.
Aangalia njia ya kuzitambua fursa katika eneo lako unaloishi.
1. Tafuta mahitaji ya watu.
Kila mahali unapoishi kwa namna moja ama nyingine watu huwa wanahitaji huduma au bidhaa fulani. Hivyo ni vyema ukaa chini na kutafakari ni vitu gani unadhani watu wanahitaji nini zaidi ? Baada ya kupata majibu ni wakati wako muafaka wa kuweza kuvisogeza kwa watu hao na wao wakanunua. Kufanya hivyo ni njia nzuri ya wewe kupata pesa. Pia watu wengi hupenda Huduma ambayo inapatikana kwa rahisi hivyo fanya uchunguzi wa kutosha na kuona watu wanapenda nini zaidi kuzisogeza huduma hizo kwa watu.
2. Toa majibu ya changamoto za watu.
Kuna swali la msingi sana la kuujiuliza juu ya maisha yako. Swali lenyewe ni kama lifuatavyo hivi ni kwa nini huna pesa? Ukipata majibu ya swali hilo ni nusu ya kupata mafanikio.
Moja ya tafiti ambazo ziliwahi kufanywa ni kwamba watu wengi hawana pesa kwa sababu kuu mbili, mosi kwa sababu hawatatui matatizo za watu. Sababu ya pili, watu wengi hawana pesa kwa sababu wanatatua matatizo machache, hivyo siri ya kubwa ya mafanikio yako ipo katika kutatua matatizo ya watu wengi katika njia ya tofauti na walivyozoea wengine.
3. Rahisisha majibu ya kazi
Watu wengi hupenda vitu ambavyo havina ugumu katika kufanya kazi, wetu wengi tunapenda kufanya kazi kwa kutumia njia rahisi na kupata majibu kamili tunayoyatarajia. Hebu angalia moja ya tajiri mkubwa dunia bwana Steve Job ambaye ni mmliki wa kampuni ya Apple, yeye alitazama jinsi watu ambavyo walikuwa wanatumia vifaa vya kietroniki kama simu za butani, desktop computer ambazo kimsingi zilikuwa ni vigumu hata kutembea nazo.
Hivyo Steve Job akaamua kutengeneza vitu hivyo hivyo kwa kuongeza thamani leo hii tunafurahia simu za apple na laptop za apple ambazo zina mambo mengi pia zinasaidia kurahisisha kazi na kuifanya dunia kama kijiji.
Kwa hiyo kama alivyofanya tajiri huyo ni wakati mwafaka kufikiri ni zipi kazi ngumu ambazo zinawakabili watu na kuweza kuzipa majibu ya ugumu huo.
No comments
Post a Comment